February 13, 2018



Kiungo wa Simba, Jonas Mkude ameachwa jijini Dar es Salaam baada ya kuchelewa ndege.

Mkude ameachwa baada ya kuchelewa wakati Simba ikiondoka kwenda Shinyanga kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mwadui FC.

Taarifa zinaeleza kuwa Mkude alichelewa ndege kutokana na kushindwa kufika kwa wakati kama ilivyotakiwa.

“Hii ni mara ya pili ndani ya miezi miwili, Mkude anachelewa na kuachwa. Hivi karibuni alionywa kutokana na kocha, tena ni kocha huyu mpya.

“Kocha anampenda Mkude lakini yeye anaanza kuharibu taratibu,” kilieleza chanzo.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic