MPIRA UMEKWISHA
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 90 sasa, wachezaji wote wa St Louis wamerudi nyuma na mpira unakuwa mgumu kwa Yanga wanaotaka bao la pili huku wageni wao wakionekana hawataki kufungwa zaidi
Dk 88 St Louis nao wanafanya mabadiliko wanamtoa Herve na kumuingiza Lane
SUB Dk 86 Yanga wanamtoa Buswita, anaingia Yusuf Muhilu kuchukua nafasi yake
Dk 85 krosi nzuri ya Chirwa, Buswita anaruka vizuri lakini St Loius wanaokoa
Dk 82, Mahadhi anaingia kwa kasi tena lakini inaokolewa na kuwa kona, inachongwa na Mwashiuya, inaondoshwa
Dk 81, Mwashiuya anaachia mkwaju mkali kabisa, goal kic
KADi Dk 80 Herve wa St Louis analambwa kadi ya njano kwa kumvuta Mwashiuya
Dk 77 kwa kuwaangalia, hawa St Louis wanaonekana wamechika sana lakini wanajitutumua. Yanga wanapaswa kuzidisha mashambulizi ili kupata bao la pili
Dk 75, MWashiuya anachonga kona lakini safai hii kipa Todo, anadaka kwa ulaini kabisa
Dk 75 pasi nyingine nzuri, Mahadhi anaiwahi lakini beki anatoa na kuwa kona
Dk 73, St Louis wanafanya shambulizi kali, mshambuliaji wao alibaki yeye na kipa Kabwili, mpira wa kichwa, akashindwa kumalizia
Dk 72, Yanga wanapoteza nafasi nyingine nzuri hapa baada ya krosi nzuri ya Mwashiuya, kumfikia Chirwa ambaye anapiga shuti kuuuuuuubwaaaaaa
Dk 70, Yondani anaachia mkwaju mkali hapa, mara nyingine kipa yuko makini
Dk 68, St Louis wanaonekana wamepania kurejesha bao, wanafanya shambulizi lakini Yanga wako makini
GOOOOOOOOOOO Dk 67, Yanga inapata bao la kwanza kupitia Mahadhi akiunganisha mpira wa kichwa uliomrudia baada ya kona ya Mwashiuya
SUB Dk 66 Juma Mahadhi anaingia kuchukua nafasi Ajibu na Martin anakwenda nje pia anaingia Godfrey Mwashiuya
Dk 64, Yanga inapata kona nyingine lakini ni dhaifu
Dk 60 Ajibu anapoteza nafasi nyingine muhimu kabisa, yeye na nyavu, hii hatari kabisa
Dk 60 St Louis wanafanya mabadiliko
Dk 56 Bado Yanga hawana ile hali ya kutaka kupata bao la mapema
Dk 52, St Louis wanafanya shambulizi kali, Yanga wanajichanganya hapa
Dk 50 sasa bado hakuna bao, Yanga wanapata kona lakini ni butu
Dk 48 St Louis inapata kona, inachongwa lakini ni dhaifu kabisa
Dk 47 Yanga wanapata kona ya kwanza kipindi cha pili, inachongwa, Buswita anapiga tik tak, kipa anadaka
Dk 45 Mechi imeanza kila upande ukionekana umepanga kufanya vizuri
MAPUMZIKO
DAKIKA 1 YA NYONGEZA
Dk 44 St Louis wanagongeana vizuri kwa lakini mwisho wanapiga shuti kuuubwa la kutungua minazi
Dk 43, Tshishimbi anaachia mkwaju mkali kwelikweli, bahati mbaya unatoka nje sentimeta chache kwenye lango la St Louis
Dk 41 mwamuzi anasimamishwa mpira kwa muda, wachezaji waweze kupoza makoo yao
Dk 40, inachongwa kona, mpira unamkuta Yondani anaachia mkwaju mwingine matata lakini hakulenga lango
Dk 39, Gadiel anaingia vizuri anapiga krosi, inaokolewa na kuwa kona
Dk 37, Gadiel anachonga kona ya tano ya Yanga, ni kona dhaifu na inadakwa kwa ulaini
Dk 37, Yanga wanapata kona nyingine, inachongwa na Ajibu, inaokolewa na kuwa kona ya tano
Dk 35, mpira safi wa Ajibu, Buswita anapiga kichwa nyanya, goal kick
Dk 34, nafasi nyingine ya Yanga, Ajibu akatika nafasi nzuri anapiga kasimama kama msumari, goal kick
Dk 33, Yanga wanasukuma shambulizi jingine na kupata kona, inachongwa kona dhaiifuuu kabisa, hawa Yanga vipi?
Dk 32 Gadiel anaichonga ile faulo la anapiga hovyo kabisa
Dk 31, beki wa St Louis anaunawa mpira nje kidogo ya boksi yao, mwamuzi anasema ni faulo
Dk 30, yanga wanagongeana vizuri na Patrick Kelvin Yondani anajaribu mkwaju maridadi kabisa, goal kick
Dk 27, Ajibu anapiga faulo hiyo lakini inatoka nje sentimeta chache juu ya lango la St Louis
Dk 27, chirwa anaangushwa nje kidogo ya boksi mwamuzi anasema faulo
ANAKOSAAAA Dk 24, Chirwa anapiga na mpira unapita nje. Iko haja ya Yanga kumbadili sasa Chirwa katika upigaji penalti
KADI Dk 22, Herve analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Kessy
PENAAAAAAAT Dk 22, Kessy anaangushwa ndani ya eneo la penalti box na mwamuzi anasema ni penaaat
Dk 19, Martin anaachia mkwaju mkali kabisa lakini hakulenga lango hata kidogo...
Dk 17, St Louis inabidi pia wawe makini maana wanacheza faulo hovyo, Yanga wanatakiwa kuendelea kuwapa presha zaidi ili wazidi kucheza faulo
Dk 17, Yanga wanaonekana kuchangamka, Buswita anaachia mkwaju mkali lakini unatoka nje kidogo
Dk 17, nafasi nyingine kwa Yanga, Chirwa anaingia vizuri lakini Yanga hakuna mtu
Dk 16, Yanga wanapata kona, inachongwa na Ajibu, nafasi nzuri kwa Buswita baada ya kipa kujichanganya lakini anachelewa
Dk 15 sasa, ndani ya dakika tatu hakuna shambulizi hata moja la Yanga ndani ya lango la St Louis. Yanga wanatakiwa kujitahidi kupata bao mapema na mfumo wa krosi wanaoutumia unaonekana umekataa, hivyo lazima wabadili ili kupata mabao ya mapema kwa kuwa wao ndiyo wako nyumbani
Dk 11, shambulizi jingine la St Louis, Tahid anaachia mkwaju mkali hapa lakini Kabwili yuko vizuri, anakamata
Dk 10 sasa, bado Yanga hawajafanya shambulizi kubwa na hali ilivyo, St Louis wanaonekana kukaa nyuma zaidi wakifanya mashambulizi ya kushitukiza
Dk 7, shambulizi kali la kwanza la St Louis, krosi nzuri lakini Tshishimbi anafanya kazi nzuri kabisa na kuokoa
Dk 5, Yanga wanapata kona, inachongwa lakini ni dhaifu, inaokolewa
Dk 3 Martin naye anageuka naye vizuri, mkwaju mkali kabisa kutoka mguu wake wa kushoto, kipa yuko makini, anadaka
Dk 2 Tshishimbi anaachia mkwaju safi hapa lakini ni goal kick
Dk 2 krosi safi ya Buswita, walinzi St Louis wanazembea na Raphael Daud anachelewa
Dk 1, mechi ndiyo imeanza na Yanga wanaanza kujipanga wakitaka bao la mapema
Hongereni Yanga. Timu imejitahidi. Muhimu sasa kujiandaa kwaajili ya mechi ya marudiano. Yanga inao uwezo wa kuwafunga kwao.
ReplyDelete