Uongozi wa Klabu ya Yanga umeonyesha hofu kufuatia uwepo wa wachezaji wengi wenye majeraha kwenye timu hiyo.
Yanga imeanza kupata hofu juu ya mchezo wao wa kimataifa ambao watavaana na St Louis Suns United ya Shelisheli wikiendi hii ambapo ilipata nafasi hiyo baada ya kuibuka mabingwa msimu uliopita.
Miongoni mwa wachezaji wa Yanga wanaoumwa ni pamoja na Donald Ngoma, Amissi Tambwe, Thaban Kamusoko, Youthe Rostand, Pato Ngonyani, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Yohana Nkomola, Mwinyi Haji, Juma Abdul na Ibrahim Ajibu.
Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, alisema kuwa, uwepo wa majeruhi wengi katika msimu huu unawaathiri kwa kuwa ni jambo ambalo halijawahi kutokea kwa muda mrefu, hivyo kunaweza kuwapa wakati mgumu katika mechi za ligi na kimataifa.
“Uwepo wa majeruhi wengi katika kikosi, unaiathiri timu kwa kiwango kikubwa katika kipindi hiki ambacho timu inahitaji matokeo katika kila mechi ili kuweza kutetea ubingwa wetu msimu huu.
“Pia itatupa shida katika mechi za kimataifa, hivyo hatuna jinsi kwa kuwa ni hali ambayo tayari imeshajitokeza hivyo mwalimu atawaandaa wachezaji waliopo kimazoezi na programu mbalimbali ili waweze kuwa fiti na kufanya vyema katika ligi na mechi za kimataifa,” alisema Ten.
0 COMMENTS:
Post a Comment