February 7, 2018



Nyanda namba moja wa Yanga Mcameroon, Rostand Youthe anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki moja sawa na siku saba akiuguza majeraha yake ya enka na hivyo ataukosa mchezo wa kwanza wa Yanga wa Kimataifa.

Mcameroon huyo, alipata majeraha hayo katika dakika ya saba na kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Rqamadhani Kabwili katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Lipuli FC mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Samora, Iringa.

Kwa maana hiyo, kipa huyo ataukosa mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika watakaocheza Jumapili hii dhidi ya St Louis ya Shelisheli kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Daktari Mkuu wa timu hiyo, Edward Bavu alisema kipa huyo atakaa nje ya uwanja kwa ajili ya kupata matibabu ya haraka yatakayomuwezesha kurejea uwanjani mapema.
“Youthe baada ya kufanyiwa vipimo na kugundulika ana jeraha dogo katika mguu wake sehemu ya enka, ametakiwa kupumzika kwa muda wa wiki moja.
“Akiwa nje ya uwanja ataendelea na mazoezi madogo huku akiendelea kupata matibabu yatakayomwezesha kupona kwa haraka ili arejee kuipambania timu yake,”alisema Bavu.

Kwa upande wa Youthe alisema kuwa “Ni kweli nitakaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki moja, niseme kuwa ninaumia kupata majeraha haya ambayo yameniharibia mipango yangu.

“Nilitaka niendelee kukaa golini kwa ajili ya kutengeneza rekodi yangu ya kudaka mechi nyingi tena kwa kiwango cha juu na kama nilivyokwambia ninataka kuwa kipa bora,”alisema Youthe.


Kipa huyo alikosa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara jana dhidi ya Njombe Mji na sasa atakosa mchezo wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya St Louis ya Shelisheli, Jumamosi ijayo.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic