Majimaji ya Songea inatarajia kukutana na mabingwa watetezi Yanga katika Uwanja wa Taifa jijini Dar, kocha msaidizi wa timu hiyo, Habibu Kondo, amefunguka kuwa walijua watakuja kucheza na wapinzani wao hao, hivyo wameshajiandaa vya kutosha.
Kocha Msaidizi wa Majimaji, Habibu Kondo, alisema kuwa walishajua kuwa watacheza na Yanga katika mchezo wa marudiano, lakini kitu kilichowafurahisha, wamepangwa nao pia katika Kombe la FA.
“Sisi tumejipanga vya kutosha kwani tulishajua lazima tutacheza na Yanga kwani timu zipo 16 na zote lazima ukutane nazo lakini pia kila mchezo wa ligi kuu ni mkubwa, hivyo sisi tumejiandaa na hapa tupo safarini kuja Dar (ilikuwa jana) kwa ajili ya mchezo huo.
“Kwanza tumefurahi kupangwa na Yanga katika michuano ya FA kwani tulipojua tumeingia hatua ya 16 bora tulijua tutapangiwa na timu yoyote, kwa hiyo sisi tumepangiwa kucheza na Yanga limekuwa jambo nzuri, kwa hiyo tupo kwenye malisho ya mechi zetu hizi mbili,” alisema Kondo.







Maneno ya kujipa matumaini bado Yanga ni timu bora dhidi ya majimaji
ReplyDelete