7
Hemed Kivuyo
Kuizuwiya Yanga kufanya mazoezi katika Uwanja Wa Taifa wakati IPO kuiwakilisha nchi na wakati huohuo kuwapa ridhaa wapinzani wao kuufanyia mazoezi kwasababu zozote zile,ni sababu zisizo na mashiko hata kidogo.
Sababu tu wataalam Wa walotengeza kiwanja hicho wanasema usitumike kwa wiki nzima,ni sababu dhaifu mno pamoya na utaalamu wao.
Kama nikweli wataalam wanaona Uwanja huo kutumika utaharibika basi hao wataalam watazamwe upya kuhusu "utaalam wao". Kama Uwanja unajengwa na haikidhi ama haumudu kuchezewa kwa wiki nzima basi huo siyo Uwanja Wa Kandanda labda wakufanyia "siasa".
Hivyo viwanja tunavyoona ambavyo nibora zaidi ya huu Wa Taifa vinatumika kila siku_vinachezewa ligi,vinachezewa michuano ya Ulaya nk siyo viwanja hivyo?? Mbona vinabaki na ubora wao!!
Kama Uwanja Wa Taifa umekarabatiwa,kwa maana ya kuboreshwa halaf unalelewa kwakutokuchezawa kama ilivyo katika nia yakujengwa basi kuna shida bila kujali sababu zozote dhaifu!
Hii ni ishara bado suala ama neno "Uzalendo "limetupita mbali sana..
Siyo Mara moja timu ya taifa ama vilabu vya Tanzania vinafanyiwa visa vya kunyimwa Uwanja Wa mazoezi wanapokuwa nje,Mara hii Yanga inakutana na visa hivyo nyumbani kwao. Ajabu sana!!!
Huu uwanja ili ulelewe vyema kwa mujibu Wa hao watalaam ni afadhali ufungwe! Majani yastawi..ifanyiwe shughuli inayoonekana inafaa.
Kuelekea pambano hilohilo msemaji Wa Simba anawasihi wanasimba kuishangilia Yanga siku ya jumamosi dhidi ya wageni. Kunasababu mbili ama Tatu zilizomfanya aseme hivyo..
.mosi,msemaji huyo anajua ama anadhani mchezo huo mchezo mwepesi kwa Yanga,kivyovyote Yanga wataibuka na ushindi.sasa anawahadaa mashabiki Wa Yanga ili wakaipe Simba nguvu siku ya jumapili ambayo anahisi kwao itakuwa mlima.
Pili ,anajua suala la mashabiki Wa Yanga kuishangilia Simba ama Simba kuishangilia Yanga haliwezekani.
Wanayanga waachane na "propaganda" hizo waende wakashangilia wapinzani Wa Simba jumapili..huo ndiyo utamu Wa soka ingawa siyo uadui. Sidhani kama angesema hivyo kama Yanga ingalikuwa inavaana na El-hilaly...
Lipo tatizo
ReplyDeleteKivuyo naye kumbe ni kama mbolembole tu, hii analysis ni ya kitoto kabisa na ni upuudhi mkubwa kwa mtangazaji Wa kituo kinachoheshimika kabisa kutoa analysis ya kishamba kama hii.
ReplyDeleteTatizo ni shule!!! Kusoma kwa kukariri badala ya kuelewa halafu mtu anajiita kioo cha jamii
ReplyDeleteTatizo linalomtafuna kivuyo ni unazi na mahaba aliyonayo kwa klub ya Yanga. ametoa uchambuzi wake kama shabiki na mwanachama wa klubu anayoipenda `yanga. Pole sana Kaka ila unapaswa kutambua usipende kutoa analysis kwa kitu ulichokuwa na masihi nacho kwasababu utakachokieleza hakiendana na uhalisia. Jifunze kuondoa hasira wakati wa kuandika habari
ReplyDeleteMuflis ubora wa kitu matunzo
ReplyDelete