February 17, 2018


Kwa misimu miwili mfululizo, kiungo Thabani Kamusoko alikuwa ndiye gumzo zaidi katika klabu ya Yanga.

Kamusoko alikuwa ni kipenzi cha mashabiki wengi wa Yanga kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa akiuonyesha raia huyo wa Zimbabwe.

Lakini mambo yanaonekana yamebadilika na nafasi hiyo kwenye mioyo ya mashabiki wa Yanga, imekwenda kwa kiungo Papy Tshishimbi raia wa DR Congo.

Tshishimbi sasa ndiye kiungo gumzo na kipenzi cha mashabiki wa Yanga tena kwa kiasi kikubwa.

Kiungo huyo amekuwa gumzo kutokana na namna anavyopambana katika ukabaji pia kuichezesha timu.

Kama haitoshi, Tshishimbi amekuwa mzuri katika ufungaji wa mabao na mengi yakiwa ni yale ya mashuti makali.

Wakati fulani, Kamusoko alikuwa akisifika kwa upigaji mashuti ambayo sasa yanapigwa na Tshishimbi.


Suala la majeruhi mfululizo, ndiyo linaonekana kumuangusha Kamusoko ambaye hata hivyo ameendelea kuonyesha nidhamu na ushirikiano wa juu kwa wenzake na benchi la ufundi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic