![]() |
| Adam Juma |
Mtoto anayejulikana kwa jina la Adam Juma, amekabidhiwa jezi rasmi ya mchezaji huyo anaiyechezea klabu ya Simba.
Juma ambaye picha zake zilionekana katika mitandao mbalimbali ya kijamii akiwa amevaa fulana ya kawaida huku ameichora kwa jina la Okwi, amekabidhiwa jezi hiyo na kiongozi wa makundi ya Simba mitandaoni, Josee Mnyama.
Imekuwa ni kawaida sasa kwa wachezaji wa Ligi Kuu Bara kuwapatia watoto jezi zao rasmi pale inapotokea wanaonesha mahaba ya kuandika majina yao kwenye nguo zao.
Tukio hili si la kwanza, kwani iliwahi kutokea pia kwa Ibrahim Ajibu kumzawadia jezi mtoto, wakati huo akiwa Simba.








0 COMMENTS:
Post a Comment