RUVU SHOOTING YAIPAPASA HASWAA MTIBWA SUKARI, MASAU ASEMA SASA NI MWENDO WA DOZI TU
Na George Mganga
Kikosi cha Ruvu Shooting kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya walima sukari, Mtibwa Sugar FC, mechi ikipigwa katika Uwanja wa Manungu, Morogoro.
Walikuwa ni Mtibwa ambao walijipatia bao la kwanza kupitia Mhesa katika dakika ya 40, na baadaye Ruvu Shooting wakasawazisha kupitia Baraka Mtuwi 45 na Issa Kanduru kuongeza la pili dakika ya 76.
Saleh Jembe kupitia ripota wake ilizungumza na Afisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire, mapema tu baada ya mchezo kumalizika, naye alipesa walienda Manungu kufanya mpapaso kama ambavyo waliahidi.
"Tuna mfumo mpya wa kupapasa, hivyo kilichotupeleka Manungu tumekikamilisha, na huu sasa utakuwa mwenendo wa kila anayekutana nasi lazima tumpapase pia", alisema Bwire.
Kwa matokeo hayo sasa Ruvu Shooting imefikisha alama 23 na kupanda mpaka nafasi ya 7 ya msimamo wa Ligi, huku Mtibwa Sugar ikisalia na alama zake 29 ikiwa nafasi ya 6.







Pretty good post. I just stumbled upon your blog and wanted to say that I have really enjoyed reading your blog posts. Any way I'll be subscribing to your feed and I hope you post again soon. Big thanks for the useful info.
ReplyDeletedomeinnamen