FULL TIME
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 90, Njombe hawana mpango wowote na Yanga wanapunguza kasi ya mpira kwa kuwa kwao nne zinatosha
SUB Dk 88, Chirwa anakwenda benchi na kinda mwingine Said Mussa anachukua nafasi yakeGOOOOOOOOOO Dk 86, Chirwa anafunga hat trick akiunganisha pasi nzuri ya Akilimali
Dk 85 inaonekana kama Njombe mji wamekubali na wanachofanya ni kuzuia wasifungwe mabao zaidi
SUB Dk 84, Baruan Akilimali, kinda huyo anaingia kuchukua nafasi ya Martin
Dk 82, Nchimbi anaingia vizuri na kupiga mkwaju mkali lakini wapi
Dk 80, Yanga inapata kona, inachongwa vizuri hapa lakini kipa anadaka vizuri kabisa
Dk 73, krosi nzuri, Tshishimbi anajipinda lakini kidogo alishindwa kulenga lango
GOOOOOOOOO Dk 69, Martin anaandika bao la tatu baada ya mkwaju wa Mahadhi kugonga mtabaa wa panga na kurudi uwanjani
Dk 66, Kinachoonekana kama difensi ya Njombe wameishapoteana na hawana uhakika na wanachofanya
GOOOOOOOOOOOOO Dk 64 Chirwaaaaa, anafunga penalti maridadi kabisa
PENAAAAAAAAT Dk 63 Mpira wa kichwa, Ahmed anashika na mwamuzi anasema penalti na kumlamba kadi ya njano
Dk 59 kuna mchezaji wa Njombe yuko chini anatibiwa
SUB Dk 58, Njombe wanamtoa fowadi na kumuingiza, wanaingiza kipa
SUB Dk 57 Yanga wanamtoa Daud na nafasi yake inachukuliwa na Mahadhi
KADI NYEKUNDU Dk 54 kipa wa Njombe analambwa kadi nyekundu baada ya kudaka nje ya 18
Dk 49, inachongwa kona nyingine, lakini Kabwili anaidaka kwa ustadi mkubwa
Dk 48 Kabwili anafanya kazi ya ziada kuokoa shuti la Etienne, inakuwa kona, inachongwa na kuwa kona tena
GOOOOOOOOO Dk 46, Buswita anaambaa pembeni na kuachia krosi safi inayomkuta Chirwa na kuukwamisha vizuri kabisa wavuni
Dk 45 Yanga wanakuwa wa kwanza kufika kwenye lango la Njombe, wanaokoa
MAPUMZIKO
DAKIKA 1 YA NYONGEZA
Dk 44, shambulizi jingine la Yanga, kipa anapotea lakini Njombe wanaokoa
Dk 42, Yanga wanapata kona, Martin anaichonga na Njombe wanaokoa gila kick
Dk 41, Yanga wanagongeana vizuri lakini wanafanya ubishoo wa pasi za visigino, wanapoteza
Dk 40, Nchimbi tena anaachia mkwaju lakini unakuwa nyanya kwa Kabwili
Dk 37 Gadiel anaingia vizuri lakini krosi yake inaokolewa kutoka katikati ya lango la Njombe
Dk 35, Yanga wanapata kona fupi, Tshishimbi anaachia mkwajua mkali hapa, goal kick
Dk 33, Yanga wanapata kona nyingine, inapigwa na Martin lakini inavuka upande wa pili
Dk 31 kona inachongwa vizuri haoa...mwisho unaokolewa
Dk 30, krosi ya Nchimbi, shuti kali linapogwa lakini Kabwili na kuwa kona
Dk 26, nafasi nyingine kwa Njombe Mji, shuti kali la Nchimbi linaokolewa
Dk 25 Martin anaachia mkwaju mkali sana, unampita kipa tobo lakini mabeki wanawahi na kuokoa
Dk 24, dakika zinayoyoma na mpira bado unachezwa zaidi katikati ya uwanja
Dk 20 sasa, inaonekana mpira unachezwa katikati ya uwanja
Dk 17, Yanga wanaingia vizuri, kipa Njombe analazimika kutoka na kuokoa
Dk 15, Gadiel anaingia vizuri anapiga krosi, inazuiliwa na kuwa kona
Dk 10, kipa Njombe analazimika kutoka nje ya eneo lake na kuokoa mpira miguuni mwa Buswita
Dk 7 Yanga wanaingia tena, nafasi nzuri kwa Buswita lakini anapiga shuti mtoto
Dk 6, Ditram Nchimbi anamtoka Gadiel ambaye anamuwahi na kutoa nje. inakuwa kona, inachongwa goal kick
Dk 5, shuti la Chirwa linatinga wavuni, lakini mwamuzi anasema ilikuwa ni offside
Dk 3 Yanga wanafanya shambulizi kali hapa, lakini wakati Buswita akienda kuutupia mpira wavuni, beki anawahi na kuokoa
Dk 2 mpira unaonekana haujatulia na kila upande unajipanga ikiwa ni pamoja na kuwasoma wapinzani
Dk 1, Mechi imeanza kwa kasi na Njimbe mji wanafika kwenye lango la Yanga lakini halikuwa shambulizi kali
0 COMMENTS:
Post a Comment