February 2, 2018



Katika hali isiyotarajiwa, mdau mkubwa wa Singida United, Mwigulu Nchemba ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani, juzi Jumatano aliondoka uwanjani baada ya kutotaka kushuhudia timu yake hiyo ikipigiana mikwaju ya penalti na Green Warriors.

Mwigulu alikuwa mmoja wa viongozi waliojitokeza katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar kwa ajili ya kushuhudia pambano hilo la Kombe la Shirikisho (FA) ambapo Singida United walishinda kwa penalti 4-3 dhidi ya Green Warriors.

Waziri huyo alikuwa uwanjani hadi dakika ya 80 ambapo matokeo yalikuwa 0-0 kabla ya kuondoka uwanjani kwa kile ambacho kinadaiwa kuwa hakutaka kuona timu yake hiyo ikipigiana penalti ambapo alienda kuangalia kwenye runinga baada ya kutoka.

Licha ya kuondoka Singida United inayofundishwa na Kocha Hans van Der Pluijm ilifanya kweli na kupata ushindi huo wa penalti ambao unawafanya kwenda hatua ya 32 Bora ya kombe hilo. Penalti zao zilifungwa na Kiggi Makasi, Kenny Ally, Elinyesia Sumbi na Miraji Adam.


Mwigulu amekuwa msaada mkubwa ndani ya kikosi hicho ambapo amechangia kwa kiasi kikubwa usajili wa wachezaji kama Tafadzwa Kutinyu, Shafiq Batambuze, Malik Antiri, Danny Usengimana na Michel Rusheshangoga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic