February 19, 2018



MUNICH, Ujerumani
MSHAMBULIAJI wa Bayern Munich, Robert Lewandowski, juzi alipiga penalti katika dakika ya 91 na kuwapa Bayern Munich ushindi muhimu kwenye Ligi Kuu ya Ujerumani, Bundesliga.

Bayern walifanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Wolfsburg, huku mashabiki wa ligi hiyo wanaotumia king’amuzi cha StarTimes wakiishuhudia timu hiyo ikishinda mchezo wa 13 mfululizo na kuweka rekodi mpya kwenye ligi hiyo.

Kwa sasa timu hiyo yenye rekodi kwenye Ligi Kuu ya Ujerumani, imekaa kileleni kwa tofauti ya pointi 21, ikiwa na asilimia kubwa ya kutwaa ubingwa msimu huu.

Bayern kwa kuwa wanatarajiwa kuwavaa Besiktas kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kesho, iliwapumzisha mastaa wake kadhaa kwenye mchezo wa juzi.

Mshambuliaji wa Wolfsburg, Daniel Didavi, alianza kuifungia timu yake huku staa wa Bayern, Arjen Robben akikosa penalti kipindi cha kwanza.
Sandro Wagner, ndiye alianza kuwa shujaa wa Bayern baada ya kuwasawazishia katika dakika ya 64, kabla Lewandowski hajafunga la pili kwa mkwaju wa penalti mwishoni kabisa mwa mchezo huo.

Hii ina maana kuwa Bayern kwa sasa wana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Bundesliga kwa mara ya sita mfululizo.

"Jambo zuri ni kuhakikisha kuwa tunapata ushindi, hii inaonyesha kuwa timu hii ni bora na inaweza kupambana na mwishoni tukafanya vizuri zaidi,” alisema nahodha wa Bayern, Thomas Muller.

Kocha wa Bayern, Jupp Heynckes alipanga kikosi dhaifu ambapo aliwaweka nje mastaa wake David Alaba, Jerome Boateng, Mats Hummels, Joshua Kimmich, Muller huku Lewandowski akiingia akitokea kwenye benchi.

Mchezo mwingine uliwashuhudia Schalke wakikwea hadi nafasi ya tano baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Hoffenheim wakiwa nyumbani.
Cologne waliendelea kuwa na hali mbaya baada ya kutoka sare ya bao 1-1 nyumbani kwao dhidi ya Hannover.
Mshambuliaji Yuya Osako alikuwa wa kwanza kuwafungia Cologne, kabla Niclas Fuellkrug hajawasawazishia Hanover.

“Tumekuwa tukipambana kila siku kuhakikisha kuwa tunapata matokeo mazuri, naamini kuwa bado tunaweza kufanya vizuri sana kwenye michezo inayokuja, wala hatuna shaka na hilo,” alisema Osako raia wa Japan.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic