Leo Yanga inashuka dimbani ugenini dhidi ya Ndanda FC kwenye Uwanja wa Nangwana Sijaona mjini Mtwara.
Mmoja wa washambulizi watakaotaka kuiangusha Yanga ni Mrisho Ngassa.
Ngassa ni moja kati ya wachezaji walioitumikia Yanga kwa mafanikio makubwa kipindi cha nyuma na leo atakutana nao kwa mara ya kwanza baada ya kusajiliwa kwenye dirisha dogo na Ndanda FC na amefunga bao moja tu tangu asajiliwe.
Amesema; “Tunahitaji matokeo mazuri na binafsi nahitaji kulinda heshima yangu na ya watu wa Mtwara waje kwa uwingi kuona kile ambacho tutawapa wapinzani wetu watanisamehe kwa hilo.”
“Na ukizingatia wananchi wa Mtwara wamenipa zawadi toka nifikie hapa na hivyo ninaamini kesho nikijituma kwa bidii nitafanya mambo mazuri ambayo yataibeba timu yangu,” alisema mshambuliaji huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment