February 13, 2018




Kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima, ameondoka nchini na kwenda India kufanyiwa matibabu kufuatia kusumbuliwa na majeraha ya enka yaliyomuweka nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi miwili sasa.

Niyonzima aliyejiunga na Simba msimu huu akitokea Yanga, atakaa nchini India mpaka atakapokuwa fiti kabla ya kurejea hapa nchini kuitumikia timu yake ya Simba ambayo inaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 41.

 Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, alisema Niyonzima aliondoka tangu Ijumaa iliyopita na atakuwa huko akifanyiwa uchunguzi wa kina kubaini tatizo linalomsumbua.

“Ni kweli Niyonzima amekwenda India kufanyiwa matibabu na akiwa huko atakuwa chini ya uangalizi maalum wa madaktari watakaokuwa wakilitatua tatizo lake hilo linalomsumbua,” alisema Manara.


1 COMMENTS:

  1. Simba mnafanya vizuri kuwahudumia wachezaji wenu wanaoumia. Huku ndiko kujali afya za wachezaji. Hongereni sana viongozi wa Simba. AZAM pia wana utaratibu huo Hongereni.Niwaombe timu nyingine nazo wafanye hivyo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic