February 13, 2018


MAU BOFU

Kamati ya Nidhamu iliyokutana Jumamosi Februari 10, 2018 na kuamua mambo kadhaa na moja wapo ni hili; 

Mechi namba 128 (Ruvu Shooting 0 vs Simba 4). Mchezaji wa Ruvu Shooting, Mau Bofu amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kumpiga kiwiko Emmanuel Okwi wa Simba katika mechi hiyo iliyofanyika Februari 4, 2018 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 37(3) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.

Kabla Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire alisema Bovu hakuwa amekusudia na kawaida yake ni mtu mkimya asiye na tatizo.

Masau anaamini kijana huyo kamwe hawezi kumsababishia maumivu Okwi tena kwa makusudi.

 Mechi namba 123 (Singida United 3 vs Mwadui 2). Kocha wa makipa wa Mwadui, Lucheke Gaga amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada ya kuondolewa kwenye benchi (ordered off) na Mwamuzi kwa kutoa lugha ya matusi katika mechi hiyo iliyofanyika Februari 3, 2018 kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 40(11) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Makocha.
1 COMMENTS:

  1. Unawezaje conscious yako ukatetea kitendo cha kikatili cha kumpiga mchezaji mwenzie kiwiko na kuhatarisha uhai wake? Unatetea uuaji hapana viongozi wa timu kemeeni tabia hizo za ovyo kabisa si za kutetea. Mpira ni burudani sio vita.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV