February 14, 2018




Serikali ya Tanzania imezungumzia ujio wa Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Gianni Infantino ambapo imesema ipo tayari kushirikiana na Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) katika mapokezi.

Mbali ya kushiriki katika mapokezi ya ujio wa kiongozi huyo wa soka ambaye ataambatana na Rais wa Shirikisho la Soka la Afrika (Caf), Ahmad Ahmad pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli atakutana na viongozi hao wa soka.

Akizungumza juu ya ujio wa viongozi hao ambao wanatarajiwa kutua nchini Februati 22, mwaka huu, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe alisema Rais Magufuli anaunga mkono michezo na aina ya uongozi wa viongozi hao na ndiyo maana yupo tayari kukutana nao.

Waziri Mwakyembe amesema kuwa uongozi wa Fifa na ule wa Caf wa sasa upo makini katika utendaji wa matukio yake ndiyo maana umeendana na utendaji wa Rais Magufuli, hivyo uamuzi wa Fifa kuja nchini Tanzania ni sifa kwa taifa kwa sababu imeonyesha wana imani kubwa na aina ya uongozi wa TFF na ule wa serikali kwa jumla.

“Rais Magufuli amekuwa akisapoti michezo na kuwa na nia ya kuona inafanya vizuri kimataifa, hivyo ndivyo ilivyo katika uongozi wa Fifa na Caf, yawezekana hiyo ni sababu iliyochangia wao waichague Tanzania.

“Ni ugeni mzito na ndiyo maana kuna marais na makatibu wengi wa mashirikisho mengine watakaokuja pamoja na msafara huo.

“Muhimu ni kuwaunga mkono, kuwapokea vizuri ili kulitangaza vizuri taifa letu,” alisema Mwakyembe.

Katika mkutano huo wa waziri na wahariri wa michezo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Uwanja wa Uhuru, pia kulikuwa na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa, Leodegar Tenga, Rais wa TFF, Wallace Karia ambao walipata nafasi ya kuzungumza pia Makamu wa Rais wa TFF, Michael Wambura naye alikuwepo.

Akizungumzia ujio huo, Karia alisema wao wapo tayari na maandalizi yanaendelea vizuri, aliishukuru serikali kwa kuwaunga mkono na kuwa tayari kushiriki katika mapokezi.


Tenga naye alizungumzia juu ya umuhimu wa ujio huo kwa kusema viongozi hao wanakuja kwa ajili ya semina, watatokea Nigeria, hivyo amewataka Watanzania kuwapokea vizuri kwa kuwa kuna nchi nyingi zilihitaji ugeni huo lakini Tanzania ndiyo imechaguliwa, hivyo ni vema kukaonekana utofauti wa kwa nini imechaguliwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic