February 21, 2018



Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya (Uefa Champions League) inaendelea tena usiku wa leo kwa michezo miwili kuchezwa.

Baada ya ushindi dhidi wa mabao 2-0 dhidi ya Huddersfield katika kombe la FA, Manchester United itakuwa mgeni wa Sevilla leo huku kiungo Paul Pogba akirejea.

Pogba alikosekana kwenye mchezo huo kutokana na hali ya kiafya kuwa si nzuri kwake hivyo ikalazimika asicheze.



Mbali na Pogba, Zlatan Ibrahimovic naye amerejea leo mazoezini lakini hakuna matarajio kama atahusika katika mchezo wa leo.

Aidha Phil Jones, Marcos Rojo na Marouane Fellain nao wana dalili ya kuukosa mchezo wa leo sababu ya kuwa majeruhi pia.

Mechi nyingine itakayochezwa usiku wa leo ni Shaktar Donetsk ya Ukraine ambayoitakuwa mwenyeji dhidi ya Roma kutoka Italy.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic