February 18, 2018
Kikosi cha Simba kimeonyesha sasa kweli mambo yake yamebadilika baada ya kufikia katika Hoteli ya nyota 5 nchini Djibouti.

Simba imefikia katika hoteli ya Sheraton, ambayo ni moja ya hoteli kubwa zaidi nchini humo. Hoteli hiyo iko katika ufukwe wa Bahari ya Hindi.

Simba iko nchini humo kwa ajili ya mechi yake ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Gendamarie.

Katika mechi ya kwanza jijini Dar es Salaam, Simba ilishinda kwa mabao 4-0. 
1 COMMENTS:

  1. Hiyo ndio hadhi ya Klabu kubwa kama Simba, Yanga, Azam. Lazima kulinda hadhi zenu mnapoiwakilisha nchi yetu. Hongereni Simba.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV