February 18, 2018


Wachezaji na makocha Coastal Union wametuzwa kwa kupambana na kuirejesha timu hiyo katika Ligi Kuu Bara.

Mdau Nassor Bin Slum ndiye aliyewaandalia hafla na tuzo hizo.

Bin Slum ambaye ni mmiliki wa kampuni namba moja ya kuuza matairi nchini, ni mdau mkubwa wa Coastal Union.

Katika hafla hiyo wachezaji walionekana kuwa ni wenye furaha kubwa kutokana na tuzo waliyopewa.

Kocha wao, Juma Mgunda ambaye alituzwa, alifurahia kwa thamani kubwa waliyopewa.

“Sijawahi kupewa tuzo zaidi ya medali ya mshindi wa pili wa Chalenji. Lakini leo nina kumbukumbu yangu na hili ni jambo kubwa sana kwa sisi watu wa mpira,” alisema.







0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic