February 17, 2018



Beki mwenye kasi wa Simba, Shomari Kapombe amewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuwa, wasiogopeshwe na sare dhidi ya Mwadui FC ambapo amesisitiza kuwa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwao bado upo palepale.

Kapombe aliitoa kauli hiyo mara baada ya sare ya mabao 2-2 na Mwadui juzi Alhamisi kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Licha ya kutoka sare hiyo, Simba imebaki kileleni katika msimamo wa ligi wakiwa na pointi 42 huku Yanga wakifuatiwa wakiwa na pointi 37.

Kapombe alisema mashabiki wa Simba wasikatishwe tamaa na matokeo hayo waliyoyapata kwani bado wana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu.

Kapombe alisema kikubwa ni mashabiki wa timu hiyo waendelee kuisapoti timu hiyo kwa kuendelea kujitokeza uwanjani kwa ajili ya kuwashangilia ili waendelee kupata matokeo mazuri.


“Ni ngumu kwa timu kuendelea kupata matokeo mazuri kwenye mechi za ligi, kwani wapinzani wetu nao wanajiandaa kupata ushindi ila matarajio yetu ya ubingwa bado yapo palepale.

“Ushindani kama unavyouona wa ligi msimu huu, timu zote zimejiandaa kwa ajili ya kuchukua ubingwa na nyingine kutaka kumaliza ligi katika nafasi nzuri na ndiyo sababu ya sisi kupata sare na Mwadui.


“Kikubwa mashabiki wetu wasikate tamaa baada ya matokeo hayo, tunajua matokeo yamewaumiza lakini watarajie kupata matokeo mazuri kwenye michezo ijayo,” alisema Kapombe.

SOURCE: CHAMPIONI

2 COMMENTS:

  1. Kapombe tunakuelewa unachokisema lakini wapenzi na mashabiki lazima tuwe na hofu maana huko nyuma tumeshapitia hayahaya tumeongoza kwa pointi 8 baadae zikafululiza drooo zikatengeneza kabati. Hatutaki tena experience hiyo. Mwadui mnecheza kwa nguvu muda wote tungewafunga goli 4. Lakini kuna wakati mkacheza show game hata kocha mfaransa nilimuona anang'aka mnafika golini kwa mpinzani halafu mnarudisha nyuma kabisa mpira badala ya kutafuta goli mbele. Simba mna uwezo mkubwa sana lakini mnacheza wakati mwingine kama mechi ya kirafiki au mazoezi hivi. Badilikeni wachezaji wetu tunataka magoli hata kama 10. Kiwekeeni malengo ya magoli 4 kila timu mnayopambana nayo. Mnaweza. Msicheze bila kujiwekea malengo ya magoli mangapi .

    ReplyDelete
  2. OK sawa tunaomba muoengeze kasi ya ushindi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic