February 24, 2018


Na George Mganga

Singida United imejiunga na Njombe Mji FC katika hatua ya 8 bora ya Kombe la Shirikisho, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Polisi Tanzania.

Katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Namfua mjini Singida, ulishuhudiwa dakika 45 za kwanza zikienda sare ya suluhu bila kufungana.

Baada ya kipindi cha pili kuanza, dakika 70 kwa Kennedy Juma aliiandikia Singida United bao la kwanza, na bao hilo lilichuka dakika 7 tu, ambapo dakika ya 77 Tafadzwa Kutinyu, aliandika bao la pili na kufanya Singida iwe mbele kwa mabao hayo.

Mpaka dakika 90 zinamalizika, Singida United 2 na Polisi Tanzania 0.

Singida imekuwa timu ya pili sasa kuingia hatua ya nane bora katika mashindano hayo, baada ya Njombe Mji kuwa wa kwanza, kufuatia ushindi dhidi ya Mbao FC.

Baadaye majira ya saa moja, KMC FC itakuwa inacheza dhidi ya Azam FC, kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic