February 28, 2018


Na George Mganga
 
Licha ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ndanda FC jioni ya leo, mashabiki na wanachama wa Yanga wamemlalamikia kipa wao Youthe Rostand kutokana na kiwango anachokionesha.

Ukiachana na Mjumbe wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali, kuanza kumnyooshea kidole kipa huyo, baadhi ya mashabiki wamekuwa wakihoji inakuwaje kiwango cha kipa huyo kinashuka.

Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Facebook na Instagram, wapo wale walioandika ni muda sasa wa Ramadhan Kabwili au Beno Kakolanya kupewa nafasi ya kucheza nafasi yake.

Hivi karibuni kipa huyo aliyesajiliwa kutoka African Lyon iliyoshuka daraja msimu uliopita, amekuwa hafanyi vizuri tofauti na alivyokuwa akicheza mwanzo.

Mashabiki hao baadhi wamefikia hatua ya kulishauri hata benchi la ufundi kwa kushawishi litoe nafasi kwa Kabwili ama Kakolanya ambaye hajacheza muda mrefu.

Mbali na lawama hizo kutoka kwa mashabiki na viongozi, benchi la ufundi chini ya Kocha, George Lwandamina, limeendelea kumtumia Rostand kama kipa namba moja wa timu hiyo.

3 COMMENTS:

  1. Jamani tuheshimu kazi ya kocha mkuu na benchi lake la ufundi. Tusiingilie kwenye kupanga timu chondechonde

    ReplyDelete
  2. Huyo golikipa hafai na kiwango chake hakifanani kabisa na professional, makosa kila Siku ni Yale Yale ya kutokea mipira bila kuwa na uhakika wa kuidaka, alifanya kosa kama hilo kaitaba, kafanya na st Louis kule sheli sheli, kafanya na majimaji na kaja kufanya kwa ndanda. Mwili mkubwa uwezo hafifu sana, huyo ni wa kumtema tu next time.

    ReplyDelete
  3. Kuna magolikipa wengi wa tz wazuri kuliko huyo, mfano yule golikipa wa Zanzibar aliyecheza challenge Kenya, kuna Anthony Agathon mkando wa lipuli,nk ni wazuri sana tena sana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic