February 25, 2018


Kwa kweli Ibrahim Akilimali ndiyo mtani hasa wa Simba na wenyewe wanalijua hilo, maana akiibuka tu dhidi ya ni "dongo".

Mzee Akilimali anaamini Simba kukutana na Al Masry ya kisri katika Kombe la Shirikisho, kazi wanayo na wamepewa "chuma" hasa.

Kauli hiyo ya Mzee Akilimali imekuja baada ya Simba kutinga raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo sasa itacheza na Al Masry ya Misri Machi 6, mwaka huu.

Mmbaya zaidi, anaamini safari ya Simba kuendelea na michuano hiyo, ndiyo imeishia hapo.


 “Safari hii naona nao wamepata chuma kwa sababu miaka ya nyuma walikuwa wanatucheka kwamba hatuwezi kucheza na Waarabu nao ndiyo walikuwa wanajifanya wanawamudu kwa kuangalia historia.

 “Lakini jambo zuri wamepata bahati na wamerejea kwenye michuano ya kimataifa ila sasa wale wanaokutana nao ni chuma cha moto, Simba hawawezi kwenda popote,” alisema Mzee Akilimali. 

Al Masry ni miongoni mwa timu ambazo zinatoa upinzani mkali kwa vigogo wa soka Misri ambapo ni Zamalek na Al Ahly na sasa wapo nafasi ya nne katika Ligi ya Misri wakiwa na pointi 42.


Kocha wa Al Masry ni mshambuliaji wa zamani wa Zamalek, Hossam Hassan ambaye alikuwepo kwenye kikosi  cha Zamalek kilichong’olewa na Simba mwaka 2003 katika Klabu Bingwa Afrika.

2 COMMENTS:

  1. Mzee wetu kaongea vizuri hajatukana mtu wala klabu ametoa maoni na maono yake. Ni kweli timu za Misri kali huwezi kufananisha na timu ya Botwana. Ndio maana profile ya Simba ni kubwa kwakuwa unapopambanishwa na timu kubwa zenye majina huwa ni jambo jema unatangazika na kujulikana zaidi.Umesahau Simba ilichowafanyia Zamalek? Hiyo ndiyo Simba.

    ReplyDelete
  2. Maneno kama hayo ya kukatisha tamaa na kujidumaza kama angeongea Hanspop wa Simba angeambiwa msaliti na si mzalendo. Ukiangalia kiuhalisia yanga ana mtihani mgumu zaidi kuliko Simba licha ya kelele zote za kuitoa Simba kwenye mashindano.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic