February 25, 2018





Wakati Simba inajiandaa kuendeleza ubabe wake katika Ligi Kuu Bara, wapinzani wao, Mbao FC wanawaza mengine kabisa.

Simba ndiyo vinara wa ligi hiyo na mechi yao ijayo ni dhidi ya Mbao FC kesho Jumatatu. Lakini Mbao licha ya kuwa ugenini, wameapa kuwatuliza vinara hao.


Mbao wamesafiri kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam kucheza na Simba mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, huku wakiwa na kumbukumbu ya sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa awali.

Mwenyekiti wa Mbao, Solly Njashi, ameliambia Championi Jumamosi kuwa, kikosi chao kipo kamili kwa ajili ya kukabiliana na Simba licha ya kwamba wapo ugenini lakini wanataka pointi tatu tu.

"Sisi tupo kamili kabisa kwa ajili ya mchezo wetu na Simba na tumekuja Dar es Salaam kwa ajili ya kusaka pointi tatu, tumekuja kushangaza.


"Kocha Etienne Ndayiragije pamoja na kikosi kizima kimejiandaa madhubuti kabisa kwa ajili ya mchezo huo na tuna imani kwamba tutafanya vyema tena baada ya kutolewa katika Kombe la FA," alisema Njashi.

Mbao FC wanaamini wao hawashindwi kuwaangusha vigogo kwa kuwa katika mechi ya kwanza ya msimu huu dhidi ya Yanga, Mbao waliifunga Yanga mabao 2-0 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

3 COMMENTS:

  1. Tunawaheshimu na kuwapenda Mbao lakini wasijikweze kiasi hicho Simba na Yanga bado ni timu kubwa kwao. Wakishinda au kutoa suluhu huwa ni news lakini haitegemewi. Kesho Simba inashinda.

    ReplyDelete
  2. Wanadhan simba ndo yanga mmepata droo moja ndo makelele . mnapigwa tatu

    ReplyDelete
  3. Kesho Simba tunashinda kama kawaida yetu licha ya Ngonjera za hizo mbao
    ✌✌✌ ♨♨

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic