February 19, 2018






Vingozi na wachezaji wa Yanga, kesho watakuwa uwanjani wakiishuhudia APR ya Rwanda ikipambana dhidi ya timu ya Shelisheli katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga wameamua kwenda kuwaunga mkono APR katika mechi yao kwa kuwa wanatokea Afrika Mashariki.

"APR ni wenzetu, tutakwenda kushuhudia mechi yao kesho jioni lakini pia kuwaunga mkono maana wanatokea kwetu Afrika Mashariki," alisema Maneja wa Yanga, Hafidhi Saleh.

Yanga iko nchini Shelisheli kwa ajili ya mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya St Louis.

Katika mechi ya kwanza, Yanga iliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic