Baada ya kupata ushindi mwembamba katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya St Louis ya Shelisheli, Yanga wameendelea na maandalizi ya Ligi Kuu Bara.
Yanga wamefanya mazoezi yao kwenye Uwanja wa Polisi Kilwa jijini Dar es Salaam ikiwa ni mwendelezo wa maandalizi.
Kikosi hicho chini ya Kocha George Lwandamina kilifanya mazoezi yake hayo ikiwa ni baada ya kupata ushindi huo wa bao 1-0 dhidi ya St Louis na mashabiki wake hawakuonekana kufurahia.
Yanga inajiandaa na mechi ijayo dhidi ya Majimaji jijini Dar es Salaam lakini ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya pili dhidi ya St Louis, ugenini.







0 COMMENTS:
Post a Comment