February 24, 2018




Na George Mganga

Kikosi cha Yanga asubuhi ya leo kimeondoka kuelekea mkoani Ruvuma kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Majimaji ya mjini Songea.

Kupitia ukurasa wao wa Facebook pamoja na Instagram, Yanga imekuwa ikitumia 'Hashtag' ya Chama Tawala Cha Soka Tanzania, kutokana na Msemaji wake, Dismas Teni, kunukuliwa hivi karibuni akieleza kuwa Yanga ndiyo baba wa soka hapa nchini.

Na leo kupitia mitandao yao ya kijamii, Yanga wamekuja na Hashtag haijajulikana kwa nini imetumika, na pengine mpaka kufikia maamuzi ya kuandikwa.

Hashtag hiyo iliyoandikwa Bila Yanga Hakuna Kiki, imetumika leo ambapo Yanga ikiwa katika maandalizi ya safari kuelekea mjini Ruvuma kuikabili Majimaji FC.




Saleh Jembe itajaribu kuzungumza na Uongozi wa timu hiyo, pengine watupe ufafanuzi wa kutumia 'Slogan' hiyo. Endelea kuwa nasi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic