March 27, 2018


FULL TIME: MPIRA UMEMALIZIKA KUTOKA UWANJA WA TAIFA, STARS 2-0 CONGO

Dak ya 94, Yahaya Zayd anaingia kuchukua nafasi ya Simon Msuva
Dak ya 93, Unapigwa huku, Stars wanaokoa
Dak ya 92, DRC wanajaribu kupenyeza kulia mwa Uwanja walau kupata bao la kufutia machozi, faulo, mpira unapigwa kuelekea Stars
Dak ya 91, Manula anapiga mbele huku kuwatafuta washambuliaji

DAKIKA 90 ZIMEMALIZIKA, ZIMEONGEZWA DAKIKA 4

Dak ya 89, Shomari Kapombe amebebwa kwenye machela kutolewa nje baada ya kuumia
Dak ya 87, Mabadiliko; Kichuya anatoka Uwanjani, nafasi yake inachukuliwa na Rashid Mandawa
Dak ya 86, Gooooooli, Kichuyaa, anafunga bao la pili kufuatia kazi nzuri aliyotengenezewa na Samatta
Dak ya 85, Zimesalia dakika 5 mpira kumalizika
Dak ya 84, Kadi ya njano anapewa beki wa FRC baada ya kumchezea madhambi Ibrahim Ajib
Dak ya 82, Gadieeeel, piga shuti moja lakini linapaa juu ya lango
Dak ya 82,  Mpira ni goli kiki, Kipa wa DRC anaanza upya
Dak ya 80, DRC wanapambana kupata bao hapa, Stars wanaondoka na mpira, kwake Samatta lakini DRC wanaokoa tena
Dak ya 79, Bado DRC wana mpira
Dak ya 78, Kwenda huku mbele sasa wachezaji wa DRC na mpira, wanajaribu kutafuta bao la kusawazisha
Dak ya 77, DRC wameshaanza, Stars wanaunyaka, piga huku mbele kwake Samatta tena, unamkuta Kichuyaaaaa, kipa anadaka, ilikuwa hatari

Dak ya 74, Goooooli, Mbwana Samatta anafunga bao la kwanza kwa njia ya kichwa kufuatia krosi nzuri ya guu la kushoto kutoka kwa Shiza Kichuya, Stars 1, DRC 0
Dak ya 73, Kocha Mayanga ameshindwa kukalia kiti chake, muda wote amesimama, hii ni kuhakikisha vijana wake wanapambana
Dak ya 71, Gadiel Michael anagangwa na madaktari baada ya kuumia mguu wakati akiokoa mpira uliokuwa unaelekea kwenye nyavu za Stars
Dak ya  70, Wachezaji wa akiba wa Stars wanapasha
Dak ya 68, Mpira umesimama, Banda amekaa chini
Dak ya 67, DRC na mpira, pigwa pasi moja, mabeki wa Stars wanaokoa na mpira unakwenda nje. Unarushwa huku, Manula anadaka

Dak ya 65, Kelvin Yondan anao mpira eneo la nyuma huku, pasia kwake Kichuya, DRC wanauchukua, hatarii huku langoni mwa Stars inatokea piga nikupige na DRC wanakosa goli la wazi kabisa, yangekuwa mambo mengine muda huu
Dak ya 64, DRC walishaanza, wanatoa nje, unarushwa kuelekea langoni kwao
Dak ya 63, Bahati mbaya inaiandama Stars, Msuva anakosa kuiandika tena Stars bao, mpira unamtoka miguuni na kwenda nje, Goli Kiki

Dak ya 62, Offside, Stars wanaotoea, bado matokeo ni 0-0
Dak ya 61, Ajib anashindwa kutumia nafasi yake ya kwanza vizuri, baada ya kupiga shuti na kwenda nje ya goli
Dak ya 60, Mpira ni goli kiki, unapigwa kuelekea DRC, Manula anaanza taratibu na Yondan, pigwa mbele huku
Dak ya 59, Mohammed Issa anatoka baada ya kuumia, Ibrahim Ajib anachukua nafasi yake
Dak ya 58, DRC wako langoni mwa Stars, wanafanya jitihada za kuandika bao la kwanza, mpira unakuwa faulo, unapigwa kuelekezwa DRC

Dak ya 57, Mohammed Issa ameumia, mpira umesimama kwa muda
Dak ya 57, Goli Kiki, wakati huo Manula anawaonya wachezaji wake wazidi kuwakaba DRC, wasiwaachie
Dak ya 56, Stars wanaanza tena eneo la ulinzi, pigwa kwake Msuva huku mbele, mabeki wa DRC wanakuwa maridadi wanacheza kuokoa mpira
Dak ya 54, Ndombe anatoka upande wa DRC, nafasi yake inachukuliwa na Junior Kabananga
Dak ya 54, DRC wanakosa nafasi ya kupata bao la kwanza kufuatia shambulizi zuri, mpira unakwenda nje
Dak ya 53, DRC wanaanza eneo la nyuma

Dak ya 52, Mohammed Issa na mpira, pasia kwa Msuva, unamkuta kipa wa Congo anaokoa kwa kupiga shuti kali
Dak ya 51, Msuuuuva, piga shuti kali lakini linaishia kwenye nyavu za nje, ilikuwa ni shambulizi moja zuri kwa Stars
Dak ya 50, Nyoni anacheza madhambi, mpira unapigwa kuelekea Stars, piga huku lakini DRC wanaudaka tena
Dak ya 49, Goli kiki, DRC wanaanza
Dak ya 48, Hatarii, Samatta anamtengeneza pasi muruuua kabisa Msuva na anadondoshwa ndani ya eneo la penati boksi, Mwamuzi anasema hakuna penati.
Dak ya 47, Samatta anapasia kwake Yondani, kwake Samatta tena, mabeki wa DRC wanamchezea faulo Samatta, mpira unapigwa kuelekea DRC
Dak ya 46, Mayanga anashauriana na benchi lake la ufundi huku mpira ukiendelea
Dak ya 45, Kipindi cha pili kimeanza. Ni lala salama ya Stars kutafuta ushindi

MPIRA NI MAPUMZIKO, DAKIKA 45 ZA MWANZO ZIMEMALIZIKA


Dak ya 45, Manula anadaka shuti kali la mshambuliaji wa DRC, piga huku mbele, Msuva anakosa tena bahati, mpira unakwenda nje

DAKIKA 45 ZIMEMALIZIKA, ZIMEONGEZWA MBILI

Dak ya 43, Hatari huku katika lango la DRC, kipa anaokoa mpira, ilikuwa kidogo Msuva acheke na nyavu
Dak ya 42, Mpira ni faulo, unapigwa kuelekea Stars
Dak ya 40, Dakika zinayoyoma Stars wanajaribu kufanya mikakati ya kupenya ngome ya DRC japo inakuwa ngumu
Dak ya 39, Himid Mao anapiga pasi isiyo na malengo na kutoka nje
Dak ya 38, Mpira ni faulo, karibu na eneo la hatari la Stars, inapigwa huku, goli kiki

Dak ya 37, Msuva tenaa, anapiga kichwa lakini kinakwenda pembeni kidogo ya mtambaa panya
Dak ya 35, Mpira sasa anao Simon Msuva, anapiga kwake Samatta, kwake Kapombe, piga krosii, inatolewa nje, ni kona. Msuva anapasia kwake Kichuya, piga huku, kona nyingine, anapiga Msuva
Dak ya 33, Mpira umesimama, kuna mchezaji wa Congo ameumia. Unaanza tena, Kapombe anampasia Ndemla
Dak ya 31, Namna gani hatari pale, DRC walifanya shambulio kali lakini Stars wanaonesha umahiri, wanaokoa
Dak ya 31, Congo wanarusha mpira baada ya kutoka, rusha huku unatolewa tena
Dak ya 29, Offside! Mohammed Issa ameotea
Dak ya 27, Congo wanaanza kwa kupasiana eneo la nyuma ya uwanja, kwenda huku mbele, inakuwa faulo, Mpira unachezwa kuelekea langoni mwa Stars, Banda anapata kadi ya njano

Dak ya 26, Mpira umesimama kidogo, Issa ameumia, wakati huo Mayanga anashauriana na wachezaji wake
Dak ya 25, Stars wanafanya shambulio kali hapa, krosi ya Gadiel Michael inapanguliwa na kipa wa DRC na kutoka nje, inakuwa kona. Kona inapigwa na kipa anadaka
Dak ya 23, Kibangala anatoa nje mpira, unarushwa kuelekea DRC, Kapombe amesharusha, kwake Banda sasa, anampasia Gadiel, piga huku kumtafuta Nyoni, anampasia Faisal. namna gani anapiga krosi mkaa, mpira nje
Dak ya 22, Kichuya anapasia kwake Kapombe, anapiga krosi safi lakini inakosa wamaliziaji

Dak ya  21, Kona ya pili inachongwa kuelekea Stars. Pigwa kona moja kubwaaa inakwenda mpaka nje ya Uwanja
Dak ya 19, Banda sasa na mpira, anampasia Gadiel, Congo wanatoa. Msuva anarusha lakini inakuwa faulo. Pigwa kuelekea Stars
Dak ya 18, Issa anashindwa kupiga krosi baada ya kumtoka beki wa DRC hapa, mpira unakwenda nje
Dak ya 15, Matokeo bado ni 0-0, kila timu inafanya jitihada za kutafuta bao la mapema

Dak ya 14, Mpira anao Mao,piga mbele lakini wapinzani wanaokoa. DRC wanaanza sasa nyuma, unamkuta mshambuliaji kulia mwa Uwanja huku, piga krosi lakini inakuwa mkaa. Mpira unakuwa goli kiki kuelekea DRC
Dak ya 13, Mpira bado haujawa na makali kwa timu zote mbili mpaka sasa, hatari langoni mwa Stars, inapigwa krosi moja, unaokolewa
Dak ya 11, Faulo tena kwenda Stars, DRC walishaanza, wanapasiana eneo la kati. Bado wanao, Kapombe unamfikia, anapia shuti kurejesha mbele

Dak ya 10, DRC wanapata kona ya kwanza, wanapiga inaenda mpaka nje
Dak ya 9, DRC wanauchukua, wanapasiana eneo la nyuma, piga pasi moja mbele, mpira unatoka, unarushwa kuelela Stars
Dak ya 8, Inapigwa na kuchezwa maridadi na mabeki wa Stars, Manula anaanza na Banda, kwake Yondani
Dak ya 7, Congo wanapata faulo pembezoni kabisa mwa eneo la hatari la Stars baada ya Banda kucheza madhambi

Dak ya 6, Stars wanapata kona ya kwanza, wanaanza kwa kupasiana hapa, inapigwa krosi langoni mwa DRC lakini unapaa juu ya vichwa vya wachezaji wa Stars
Dak ya 5, Congo wanamiliki sasa, piga pasi moja kule mbele, mpira unakwenda nje, goli kiki
Dak ya 4, Kichuuya, piga shuti moja kwa guu la kushoto na mpira unakwenda nje. Stars wameanza maridadi dakika hizi za mwanzo
Dak ya 3, Msuva anachukua mpira, kwake Kapombe, piga krosi lakini kipa wa Congo anadaka
Dak ya 1, Mpira umeshaanza kutoka Uwanja wa Taifa

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic