MAREHEMU ARTHUR MAMBETA KUZIKWA KESHO JUMAMOSI BUGURUNI
Na George Mganga
Taarifa kutoka klabu ya Simba zinaeleza kuwa Marehemu Arthur Mambeta anatarajiwa kuzikwa kesho Jumamosi katika makaburi ya Buguruni yaliyopo wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.
Mpaka sasa mwili wa marehemu upo Kigamboni ambapo kesho utasafirishwa mpaka Buguruni kwa ajili ya maziko kufanyika.
Mambeta alianza kuichezea Simba ikiwa inajulikana kwa jina la Sunderland, na kifo chake kimekuja mara baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Pumzika kwa amani Arthur Mambeta
0 COMMENTS:
Post a Comment