March 2, 2018

Kikosi cha Simba kinashuka dimbani Ijumaa ya leo kucheza mchezo wa ligi dhidi ya Stand United ya mjini Shinyanga.


Na George Mganga
 
Mchezo huo utakaochezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, utakuwa wa raundi ya 20 pamoja na wapinzani wao Stand United.

Simba itaipa unafuu Yanga katika mchezo wa leo endapo itaenda sare au kupoteza kutokana na utofauti wa alama 5 ambazo wanazo, ukiangalia wote wamecheza michezo sawa.

Mpaka sasa Simba ina pointi 45 na Yanga ina 40, hivyo kwa namna msimamo ulivyo mpaka sasa, kila mmoja baina ya Yanga na Simba anaweza akutwaa ubingwa.

Vilevile Simba akishinda mchezo huu, atazidi kujiwekea mazingira mazuri zaidi ya kuwaacha watani wake wa jadi wa jadi, na kufikisha alama 48 na kuwaacha kwa alama 8.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic