March 2, 2018


Na George Mganga
 
Mkuu wa Kitengo cha habari na Mawasiliano katika klabu ya Simba, Haji Manara, amezidi kusisitiza akilitaka Shirikisho la Soka nchini (TFF), kusaidia kuwalinda wachezaji.

Haji Manara amesema inabidi TFF wawe makini na wachezaji ambao wamekuwa wakicheza michezo mibaya inayopelekea kuumiza na kumfanya mchezaji awe majeruhi.

Manara ameeleza si kwamba hawataki kupambana mchezoni, la hasha, bali waamuzi wasiruhusu faulo za ajabu zitajazopelekea kuhatarisha hali za kiafya kwa wachezaji ambao ni muhimu vikosini.

"Ni vema shirikisho likasaidia kulinda hawa wachezaji kupitia waamunzi, maana kumekuwa na rafu nyingi za ajabu ambazo zinapelekea kuwakosa wachezaji muhimu kikosini, tunakubali mchezo wa mapambano, lakini si faulo ambazo hazina maana" amesema Manara.

Hivi karibuni Simba imemkosa mchezaji wake John Bocco katika mechi mbili zilizopita baada ya kumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mwadui FC.

Vilevile Emmanuel Okwi naye aliumia katika mchezo uliopita kwa kuchezewa rafu walipokutana na Mbao FC ya jijini Mwanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic