March 18, 2018



Ukiachana na matokeo ya jana pale mjini Gaborone, Botswana, Yanga imekosa mkwanja mrefu ambao ungeweza kuendeleza maendeleo ya klabu hiyo yenye makazi yake mitaa ya Twiga, Jangwani.

Yanga imeshindwa kutwaa kitita cha Bilioni 1.3 baada ya kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, kufuatia matokeo ya suluhu (0-0) dhidi ya Township Rollers FC.

Fedha hizo ambazo hutolewa pale timu inapofuzu kuingia hatua ya makundi, sasa zimehamia upande wa pili wa wapinzani wao, Township Rollers.

Wabotswana hao wamesonga mbele kutokana na faida ya bao la ugenini baada ya kuifunga Yanga kwa magoli 2-1 jijini Dar es Salaam Machi 6 2018.

Bado Yanga wana nafasi ya kupata fedha zingine endapo watafuzu kuingia hatua ya makundi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Takribani milioni 600 huenda kwa timu zinazofuzu kuingia hatua hiyo.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic