March 18, 2018


Na George Mganga

Nahodha wa klabu ya Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro', ameweka wazi sababu iliyowafanya washindwe kusonga mbele kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga ilishindwa kufuzu baada ya kupoteza kwa jumla ya mabao 2-1 dhidi ya Township Rollers ya Botswana, kwa 'Aggregate' na kuaga rasmi uwepo wao kwenye mashindano.

Akizungumza na Azam Tv baada ya mchezo, Cannavaro alisema sababu kubwa iliyowafanya washindwe kusonga mbele ni kushindwa kutumia faida ya Uwanja wa nyumbani.

"Kikubwa mabacho kimesababisha tusiweze kusonga mbele ni kushindwa kutumia Uwanja wa nyumbani, mashindano haya unapocheza ugenini kunakuwa na mambo mengi, jambo ambalo limetugharimu'' alisema.

Licha ya kuondolewa kwenye mashindano hayo, Cannavaro amesema nguvu zao zote hivi sasa wanazihamisha katika Kombe la Shirikisho Afrika walipokuwa wanashiriki Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic