March 19, 2018

6 COMMENTS:

  1. Muheshimiwa Karia anashangaza sana na utetezi wake juu ya Ammy Minne. Watanzania wapo huru kuhoji ubora wa kiongozi yeyote yule wa taasisi ya umma. Watanzania sio kama hawapendi kilicho chao bali wanachoangalia ni uwezo mtu kulingana na majukumu aliopewa. Wasomi wangapi wa kitanzania wamerudi kutoka nje na sifa tele lakini wameahindwa kuonesha ubora wao katika vitendo. Kwangu mimi Ammy Ninje ni mtu mwenye kutafuta njia ya mkato katika kujijengea wasifa wake wa kazi. Nasema hivi kwa sababu kazi ya ukocha haina tofauti na mchezaji wa mpira ni vigumu sana machezji wa mpira kuitwa timu ya taifa bila ya kupitia ngazi mbali mbali za vilabu. Na si kupitia tu ngazi mbali mbali za vilabu bali alikuwa na mchango gani. Tanzania bado tuna uhaba wa makocha wenye uwezo hasa katika ngazi za vilabu kiasi kwamba makocha mbali mbali kutoka nchi jirani wamekuwa wakimiminika kila kukicha. Suali langu ni hili kwanini Ammy Kinje hakuona umuhimu wa kutafuta ajira katika ngazi za vilabu nchini akathubitisha ubora wake watanzania wakamuona. Tena angetafuta timu ya daraja la pili au hata la tatu maana kama atafanikiwa kuitoa timu huko hadi ligi kuu hakika hakuna mtanzania atakaehoji kama TFF itamkabidhi timu ya Taifa. Lakini sio blah blah tu. Inasemekana George Masatu anataaluma ya ukocha hasa kwa soka la vijana na si Massatu tu bali wapo Mashujaa wengi tu katika mpira wa tanzania wenye uwezo kutoa mchango wao kama watapewa nafasi.

    ReplyDelete
  2. Ionekana kwenye mpira wetu bado kuna ukoloni mambo leo.ukijuana na kiongozi tu unatafutiwa nafasi

    ReplyDelete
  3. Hii ndio TANZANIA bwana NURDIN ABDALAH,sirikali kali yetu ndivyo ilivyo na ukihoji wanakufanyia UROMA na UTUNDULISU,my self acha ni cheki hili movie sijui litaishaje.

    ReplyDelete
  4. Hoja yako ndugu Karia bado haina mantiki. Kwa system tuliyonayo ya kukuza vipaji vya wachezaji wetu bado ni mbovu sana na ni miujiza kwa kocha huyo kufanikisha.Soka la leo linahitaji manajement iliyokamilika kama wenzetu huko alikofundisha hawo vijana 15 unaosema kwa sasa wako kwenye ligi ya EPL.Ndugu Karia ujiulize huyu kocha alikuwa anafundisha soka huko Uingereza ktk mazingara gani na uhalisia upi?
    Alikuwa anafundisha vijana wa umri gani? Maana navyojua wenzetu huko Europe kuna makocha wa umri under 7, 9,15,17....nikiwa na maana kocha wa kindergeten hawezi kufundisha mwenye umri wa miaka 21 sababu saikolojia ya utoto na utineja ni tofauti.
    Hata hivyo ndugu Karia uelewe kuna makocha wa kitanzania ambao wamesomea ukufunzi hadi kwenye ngazi ya Phd na mfano kina Dr.Tiboroha hivyo asitumaanishe kuwa Kinje aliyezaliwa Ilala ndio kocha bora wa kitanzania labda kwako wewe ndugu Karia.
    Tanzania imewahi kupata makocha bora wengi kuliko hata wenzetu wa Kenya, Uganda,Burundi, Rwanda, Zambia , Malawi lkn wengi wao hawakufanikiwa na strategies zao kwa sababu ya mazingara, uhalisia na system ya FAT/TFF pamoja na na vilabu tokea makocha bora niliokuwa nimebahatika kuwaona kama baadhi yao kina Celebic,Slowamik,Guatendorf,Buckhard Pape, Geoff Hudson, Maximo(Timu ya Taifa), Victor Stansleusic, Tambwe Leya (Yanga ), Naby Camara,Popadic,Edil Silva (Simba) na makocha wazelendo kina Magram Mansoor,Mohammed Msomali, Mziray,Joel Bendera n.k. lakini walishindwa kutimiza malengo yao kwasababu ya mazingara na system yetu tuliyokariri.
    Wakati mwingine unashindwa hata kumuelewa kocha unamwachaje mchezaji kama Jonas Mkude ambaye tayari ana uzoefu wa kimataifa na tayari ameshapitia kwa makocha tofauti wa kimataifa? Unawaachaje kina Buswita, Mlipili, Mhilu for under 20/23 yrs amabao nao tayari wameshaanza kucheza ktk michezo ya kimataifa kwa kutumikia vilabu vyao?
    Sasa kocha wetu kwa kukariri kuwa mchezaji anacheza nje kama Kenya basi anaitwa kuchezea timu ya Taifa.Safari hii kuna hatari ya kupigwa zaidi ya goli saba...

    ReplyDelete
  5. Bado namuheshimu sana Kiongozi wangu huyu wa mpira wa mguu hapa nchini lakini kwenye hili anaendelea kujidhalilisha. Acha kuwaburuza watanzania kwa wewe unachokiamini kuwa bora basi wote tukubaliane nawe pasipokuwa na uthibitisho wa ubora huo unaoutetea. Nikukumbushe tu nafasi yako ni dhamana kwa niaba ya watanzania. Ukitulazimisha na kutuchagulia unavyotaka wewe na timu ikaboronga kwakweli tutakurudia wewe utupishe kwenye nafasi hiyo. Ninje nani anamjua hadi afundishe timu ya taifa? Mlifanya hivyo hivyo kwa Mkwasa hadi tulipofungwa magoli 7-0 ni aibu ya karne. Leo mnajaribisha tena kwa Ninje. Huu ubinafsi lini mtaachana nao?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic