Yaya Toure baada ya kusaini mkataba na Mkurugenzi wa soka wa Man City, Txiki
Begiristain.
Kiungo nyota raia wa Ivory Coast, Yaya Toure amesaini
mkataba mpya na Manchester City wenye thamani ya Pauni Milioni 45.
Mkataba huo wa miaka miaka mine utakuwa
ukimuingizia pauni milioni 11 kila mwaka na kumuingiza nyota huyo mwenye miaka
29 kuwa kati ya wachezaji wanaovuna fedha nyingi zaidi.
Mshahara wake wa zaidi ya Pauni 210,000 kwa wiki
utabaki kama ulivyokuwa katika mkataba uliopita.
0 COMMENTS:
Post a Comment