August 13, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa kikosi cha Yanga umeibuka na kutamba juu ya kikosi chake kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara unaoanza Agosti 22.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ndani ya Yanga, Hussein Nyika, amesema kuwa kikosi ambacho wamesajili anaamini kitaleta ushindani mkubwa.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana katika mchezo uliokuwa maalum wa kumuaga Nadir Haroub 'Cannavaro' ambaye amestaafu soka.

"Tuna imani na wachezaji ambao tumewasajili, tuna uhakika wataleta ushindani kutokana na namna walivyocheza dhidi ya Mawenzi hapa Morogoro" alisema.

Baada ya kukipiga na Namungo, kikosi cha Yanga sasa kitakuwa kinaandaa silaha zake vizuri tayari kuja kukabiliana na USM Alger Agosti 19 kwenye Uwanja wa Taifa katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.




2 COMMENTS:

  1. Yanga ilibidi kujopima kwa vikosi venye uwezo mkubwa kama ilivofanya Simba na Azam ikumbukwe timu ya Al Getia ndiyo iliyotowa kipigo kikubwa. Juu ya hilo kila la heri yimu yangu

    ReplyDelete
  2. Mwandishi unachanganya madawa - copy and paste. Yanga haikucheza na Namungo. Yanga imecheza na Mawenzi Market ni Simba iliyocheza na Namungo, para ya mwisho umejichanganya.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic