April 14, 2018




Kikosi cha Yanga kinaondoka kesho alfajiri kwenda Ethiopia kucheza mechi ya marudiano na Wolaitta Dicha, lakini timu hiyo imeiwekea ngumu Simba ikisema bado ina nafasi ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Yanga itacheza na Dicha mechi ya marudiano kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika Jumatano ijayo huko nchini Ethiopia baada ya awali kuwafunga wapinzani wao mabao 2-0 jijini Dar es Salaam.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa ndiye aliyeachiwa mikoba ya kuinoa timu hiyo na Kocha Mkuu George Lwandamina aliyejiunga na Zesco United ya Zambia.

Kauli ya Nsajigwa imekuja baada ya Simba kuifunga Mbeya City mabao 3-1 na kufikisha pointi 55 ikibakisha mechi saba huku Yanga ikiwa na pointi 47 ikibakisha mechi nane.

Tayari Kocha wa Simba, Pierre Lechantre, amesema kuondoka kwa Lwandamina kunawapa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu.

Nsajigwa alisema, ligi bado mbichi kutokana na idadi ya mechi walizobaki nazo, hivyo wana matumaini makubwa ya kutetea ubingwa wao.

Nsajigwa alisema, kikubwa wao watajipanga na kuwekea mkazo katika mechi zao zinazofuata ili washinde na kupunguza tofauti ya pointi kati yao na Simba ili kufanikisha malengo yao.

“Nani kasema kuwa tumekata tamaa ya kutetea ubingwa? Kikubwa tusubirie ligi imalizike ndiyo waanze kushangilia ubingwa lakini siyo washangilie wakati sisi tumebakiza mechi nyingi kuliko wao.

“Kingine watu wafahamu Simba wanaongoza ligi wakiwa wametupita mchezo mmoja, hivyo mashabiki wa Yanga waondoe hofu.
“Ninaendelea kukifanyia marekebisho kikosi changu kwa kushirikiana na Mwandila (Noel) katika baadhi ya sehemu ili makosa yaliyojitokeza katika mechi iliyopita yasijirudie tena,” alisema Nsajigwa.



6 COMMENTS:

  1. Nahc kama hawajiamini hata katika kufanya mabadiliko ya wachezaji. Ilikuwa haiingii akilini kumtoa Hajibu....kumuingiza Mahadhi....kumchelewesha Martini. Hii si sawa. hawa walitakiwa waanze mapema ili wafanye kaz..au wabadilishwe mapema. Mtu kama Mahadhi tunamuamini lakini anatuangusha sana ndugu yangu. Atafutiwe timu ya kwenda kumuongezea confidence...Yanga haina hela lakn wachezaji wengi hawana hadhi ya Yanga

    ReplyDelete
  2. Huyo mwengine. Ati ligi mbichi. Akina Mtibwa, Prison na Prison wanakungojeeni na Mnyama ndie ataekumalizeni mapena

    ReplyDelete
  3. Na shooting pia. Kwanini anatafutwa kochi mwengine kwani wewe hufai?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Eti na shooting pia. Mpapaso wa Masau Bwire 😂😂😂😂😂😂😂

      Delete
  4. Kama ingelikuwa ile TTF yakina Malinzi nisingekuwa na wasi wasi wowote ule juu ya ubingwa kwa Yanga licha ya matatizo yanaowakabili. Muunganiko wa Manji,genge lake lile la akina Seif Magari na Malinzi SIMBA angepoteza tu ubingwa hata kama ina ubora wa kiasi gani. Binafsi nimesikitishwa sana kaondoka kwa Lwandamila. Yule mzambia hakuna ubishi ni Kocha hasa ila kaja katika wakati Yanga haipo vizuri kiuchumi. Yule mzambia ni Kocha wa kupewa majukumu ya Timu ya Taifa kwani ni Mtu kwenye uwezo mkubwa wa kuleta mshikamano miongoni mwa wachezaji kwa kifupi tunaweza kusema anakipaji cha kuleta morali na uzendo kwa wachezaji.

    ReplyDelete
  5. Hahahaa. Jamani yanga nasikia inamnyembelea Masoud DJumba msaidizi wa kocha wa Simba Mfaransa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic