April 12, 2018




Baadhi ya mashabiki na wanachama wa Yanga wamevamia ofisi za Makao Makuu ya klabu hiyo usiku huu wakimtaka Katibu Mkuu, Charles Boniface Mkwasa.

Mashabiki wamejitokeza Makao Makuu ya klabu wakimtamka Mkwasa awape ufafanuzi kuhusiana na kuondoka kwa Kocha George Lwandamina ambaye amerejea kwa Zambia kujiunga na timu yake ya zamani, Zesco United.

Baada ya kuwasili ofisini hapo, wengi wameonekana wakimtupia lawama Mkwasa, wakisema kuwa yeye ndiye chanzo cha kuondoka kwa Lwandamina kimyakimya.

Taarifa zilizoripotiwa baada ya kuondoka kwa Lwandamina, zinaeleza kuwa Mkwasa na Kocha huyo hawakuwa na maelewano mazuri haswa katika masuala mazima ya utendaji.

Mbali na utendaji, inaelezwa pia Mkwasa ana mpango wa kuachana na wadhifa wa Ukatibu Mkuu ili kuchukua nafasi ya Lwandamina.

 

7 COMMENTS:

  1. Nafikiri bundi yupo kibaa anakaribia kutua jangwani

    ReplyDelete
  2. Mgogoro hauwezi kusaidia kutetea ubingwa wenu, chonde chonde Yanga

    ReplyDelete
  3. huenda mngeenda kwa mkuu wa mkoa kwa kutelekezwa na sio kwa Katibu Mkuu

    ReplyDelete
  4. Mnavamia ofisi changieni pesa klabu niende mbele acheni utoto.timu haina pesa mnamlaumu mkwasa

    ReplyDelete
  5. Mashabiki na Wanachama Yanga tulieni, papara, mihemko, na jazba zitaidhoofisha timu. Kama kuondoka mbona wameondoka wengi tu na Yanga imebaki Imara mpaka leo.Viongozi wapo nadhani nao imewagusa na nina imani wanashughulikia hilo.

    ReplyDelete
  6. Kuondoka kwa kocha isiwe sababu ya kutengeneza mgogoro utakaodhoofisha maendeleo ya timu,Nadhani kuna haja ya kuacha ushabiki wa kizamani ni vyema Wanayanga wajue kilichosababisha kuondoka na kutafuta ufafanuzi wa changamoto zinazoikabili timu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic