April 14, 2018



Beki wa kati wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ amesema anawasubiri kwa hamu washambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi na John Bocco ili awaonyeshe kazi kuthibitisha ubora wake kwa sasa.

 Simba inaongoza kwa pointi 55, nyuma ya Yanga wenye pointi 47 katika Ligi Kuu Bara na timu hizo zitakutana Aprili 29, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa ligi hiyo.

Beki huyo ambaye muda mrefu hakuwa akipata nafasi kikosini Yanga, hivi karibuni alicheza mechi ya kwanza ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Wolaita Dicha ya Ethiopia.

 Ninja pia katikati ya wiki hii alicheza mechi ya ligi kuu dhidi ya Singida United na kuifungia Yanga bao moja na kutoka sare ya bao 1-1.

Ninja alisema; “Nimekuwa nikibezwa sana ila nafasi ya kucheza imeniongezea vitu na kunifanya nizidi kuwa bora japokuwa bado sijafikia katika kiwango changu.

 “Nikipata nafasi ya kucheza dhidi ya Simba, nataka kuwaonyesha washambuliaji wao na zaidi mipira ya juu nitaicheza kwa ustadi mkubwa na naamini washambuliaji wao hawataleta madhara.”

CHANZO: CHAMPIONI

7 COMMENTS:

  1. Huuu mtoto anachekesha sana.Ama kweli ulimi hauna mfupa. Kwanza mungeifunga Singida iliuocharazwa mabao matatu na Mtibwa. Vipi muraifunga Simba wakati njaa imekushikeni hampati mishahara na huku kocha wenu tegemeo kakukimbieni kwa kukosa haki yake na Plujin pia kukupigeni chini? Ngoja umalizike msimu ujikute pekeke yako baada ya kukimbiwa na kila mchezaji.

    ReplyDelete
  2. Ninja unawatafuta ubaya waajiri wako asee, hao watu unawakabaje...kaba mmojaa mwingine anakutia njaa, hahahahahaaaa....haya tusubiri, bado wiki mbili tu sio mbali

    ReplyDelete
  3. Ninja kaongea kiuchezaji...na si kishabiki...yeye kaongelea kazi yake. Kufungwa au kutoka droo kwa mechi na timu fulani haiwezi kukufanya usiwe bora. Simba ilitoka droo na Stand...na stand hiyohiyo ikazabwa gor tatu na Yanga..sasa umegundua utofauti wa mpira unavyokwenda. Katika mfumo wa ligi ya Tanzania...hasa zinapokutana hiz timu za Kariakoo..hakuna hata mmoja anayeweza kuibeza timu pinzani. Yanga mbovu inaweza kuifunga Simba bora na watu wakashangaa. Ngoja ifike muda tuone nani ni nani

    ReplyDelete
    Replies
    1. Zile cross za Kwasi sijuiii kama ninja hatatoka na hattrick

      Delete
  4. Kina Chirwa na wengineo wataingia mitini wenda kutafuta chakula kwengineko utabaki wewe na Hajibu wako na Canavaro

    ReplyDelete
  5. Kijana hodari uwanjani ila aangalie hatakiwi kuuruhusu mdomo wake ucheze zaidi ya miguu yake.

    ReplyDelete
  6. Ngoja tuone muda ukifika

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic