April 5, 2018




Uongozi wa klabu ya Yanga umeeleza masikitiko yake kuwakosa wachezaji wake wanne kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Africa dhidi ya Welayta Dicha FC ya Ethiopia.

Kupitia Katibu Mkuu wa klabu, Charles Boniface Mkwasa, amesema kuwa itakuwa ni pigo kwao kuwakosa wachezaji ambao ni mhimili mkubwa wa kikosi cha kwanza.

Mkwasa ameeleza kupitia kipindi cha Sports HQ kupitia EFM kuwa itabidi watumie mbadala wa wachezaji wengine ili kuziba pengo la hao ambao watakosekana kwenye mchezo huo Jumamosi hii.

Wachezaji watakaoukosa mchezo huo ni Obrey Chirwa, Said Makapu, Papy Tshishimbi pamoja na beki Kelvin Yondan. 

Sababu ya kukosekana katika mechi hiyo ni kadi mbili za njano ambazo walizipita kwenye michezo iliyopita ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers FC na St, Lous FC.

Yanga bado mjini Morogoro hivi sasa ikijiandaa na mchezo huo utakaopigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa taifa.

2 COMMENTS:

  1. Hamtuvutii nacheza pira mbovu usio na mafunzo mnaboa sana bench la ufundi limezubaa Nsajigwa anatuharibia sana timu nahyi viongozi mko kimya,

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tulia bench la ufundi liko vizuri ni wachezaji wetu tu wawe makini na kadi za kujitakia zisizokuwa na ulazima.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic