April 13, 2018




DODOMA
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na Rais wa Makampuni ya StarTimes Group, Bw. Xin Xing Pang na kufanya naye mazungumzo. Mazungumzo hayo ambayo yalilenga kuimarisha Ushirikiano uliopo baina ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Kampuni ya Star Media (T) Ltd.

Katika mazungumzo hayo Mhe. Majaliwa alionyesha kufurahishwa kwake na Ushirikiano uliopo baina ya StarTimes na TBC na kuelezea matarajio yake juu ya Ushirikiano huo. “Nina matarajio makubwa sana na Ushirikiano huu kwa sababu kupitia Ushirikiano huu TBC itaimarika zaidi na kuwa na teknolojia bora zaidi”. 


Rais wa StarTimes, Bw. Pang alifika nchini kwa ajili ya kusainiana Mkataba wa Makubaliano (MoU) na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC). Utiaji saini huo ulishuhudiwa na Waziri mwenye dhamana ya Habari Mhe. Harrison Mwakyembe ambaye naye pia aliongelea upande wa Wizara anayoisimamia, “Sasa kwa upande wetu kama Wizara ni wajibu wetu kuhakikisha yote tuliyokubaliana yanatekelezwa”.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania Prof Ayoub Rioba ambaye ndiye Mwenyekiti wa bodi ya Ubia huo alisema kuwa baada ya Makubaliano hayo sasa utekelezaji utaanza mara moja na kuongeza ufanisi zaidi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic