April 11, 2018


FULL TIME

DAKIKA 3 ZA NYONGEZA

Dk 90 Kiggi anakwenda kuchonga hiyo kona, Kambale anaruka peke yake na kupuga kichwa, goal kick 
SUB Dk 89, Yanga wanamuingiza Martin kuchukua nafasi ya Chirwa


Dk 88 Kaseke anaingia mpira wake unaokolewa na kuwa kona
KADI Dk 86 Kessy anapewa kadi njano kwa kumuangusha Chukwu
Dk 84 Mhilu tena, anaingia vizuri kabisa na kutoa pasi nzuri ya Chirwa, ndani ya miguu 12 anapiga shuti kuuuubwaaaa


Dk 84 bado hakuna mipango kwa Singida United, tofauti na Yanga. Singida wanapaswa kuwa makini au watafungwa
Dk 83 zaidi mpira unachezwa katika ya uwanja na hakuna mashambulizi mengi makali
Dk 80 krosi matata ya Kiggi, lakini Kambale anafanya madhambi kwa kumuangusha Ninja
KADI Dk 79 Kadi ya pili ya njano inatoka, nayo ni kwa Singida United, anazawadiwa Chukwu
SUB Dk 78, Ajibu anakwenda nje na nafasi yake inachukuliwa na Goefrey Mwashiuya
KADI Dk 77, kadi ya kwanza katika mchezo wa leo inatoka na inakwenda kwa KAseke ambaye ameushika mpira kwa makusudi kabisa



Dk 73 mkwaju safi wa kona wa Ajibu, Manyika anaokoa na anagongwa, mwamuzi anasema ni faulo
SUB Dk 73 Juma Madhadhi anaingia kuchukua nafasi ya Buswita
Dk 73 Chukwu analazimika kulala na kuutoa nje mpira wa Mhilu, kona
Dk 71, Kaseke anagongeana vizurik na Miraj Adam, anajaribu ilikuwa ni hatari lakini goal kick
Dk 69, kona ya Ajibu, Manyika anaruka juu kabisa na kudaka kwa ustadi
SUB Dk 68, Kagoma anaingia kuchukua nafasi ya mkongwe Nizar Khalfan

Dk 68 Ndani ya 18, Chirwa anageuka na kuachia mkwaju mkali kweli, Manyika anapangua na kuwa kona
Dk 67 Mwinyi anaingia vizuri lakini krosi yake inatua mikononi mwa Manyika
Dk 66 Mhilu anachambua watu watatu, anampa Chirwa anamchambua beki mmoja, lakini hakuwa shap katika kuupiga mpira
Dk 64 Chirwa anaingia vizuri hapaaa, chini. Mwamuzi anamuambia simama ucheze mpira...Kennedy Juma alimgusa kwa mkono pia mguu akaanguka
DK 63, Ajibu anajaribu kuchambua, anaachia mkwaju mkali kabisa, goal kick
Dk 62 Chukwu anachunga kona, inatua kwa Kaseke, anamuachia Mudathir anayepiga mkwaju mkali wa chinichini, goal kick


Dk 61 mpira wa adhabu wa Chukwu, Mwinyi anaruka na kuokoa, konaa
Dk 61, kwa takribani dakika moja nzima, Singida wamekuwa wakimiliki mpira wao, Nizar Khalfan na Mudathir wakifanya wanavyotaka wao katikati ya uwanja
Dk 59, Manyika analazimika kufanya kazi ya ziada na kuondosha mpira mbele ya Chirwa aliyekuwa amepitishiwa kimo cha nyoka
Dk 57, Mhilu anaingia vizuri lakini uzoefu unamfanya kutokuwa na maamuzi sahihi
Dk 55, kwa sasa mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja ingawa Singida United kama wanapoteza muda hivi


Dk 53, Kaseke anageuka na kumtoka Mwinyi, anaingia lakini anaonyesha papara hapa na kupiga shuti hoooovyo
Dk 50, krosi safi ya Kessy lakini Juma anaokoa kwa kichwa
Dk 50 Yanga wanaendelea kusukuma mashambulizi ya kushitikkiza, lakini Singida wanaokoa na kuwa kona
Dk 48 Kambale anataka kumpita Yondani lakini anamdhibiti vizuri kabisa
Dk 47, Singida wanaingia vizuri lakini Makasi anashindwa kupiga krosi na kuanguka
Dk 45 Yanga wanaanza kwa kasi wakionyesha wamepania kusawazisha



MAPUMZIKO

- Mpira safi wa adhabu wa Ajibu, Buswita anaishaaa juuuu...ilikuwa hatari ndani ya lango la Singida

DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
GOOOOOOOOO Dk  45, Shaibu au Ninja anaruka kuunganisha kona ya ya Ajibu na kuiandikia Yanga bao safi kwa mpira huo wa kichwa


Dk 45 Manyika anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa kichwa, unamgonga beki Juma na kuwa kona
Dk 44 Chukwu anawahadaa mabeki wa Yanga, anaingai ndani ya boksi, lakini Yondani yuko makini tena
SUB Dk 43 Salum Chukwu, anaingia kuchukua nafasi ya Batambuze raia wa Uganda
Dk 42, Kambale anajaribu kuingia kwa kasi, lakini Yondani anazuia vizuri kabisa hapa


Dk 40, kinda Mhilu yuko chini pale, inaonekana aliumizwa
DK 38, Daud anaachia mkwaju mkali kabisa hapa, ilikuwa ni hatari na jaribio la kwanza Manyika akiwa langoni
SUB Dk 36, Yanga wanamtoa kipa mkongwe Ally Mustapha 'Barthez' na nafasi yake inachukuliwa na Peter Manyika
Dk ya 34: Raphael Daudi anacheza vibaya inakuwa faulo kuelekea kwa Yanga.
Dk ya 29: Yanga wanahitaji kuwa makini, Singida wanapata nafasi ya kupiga shuti la wazi lakini mpira unapaa.
Dk ya 24: Chirwa anashindwa kutumia vizuri pasi aliyopewa na Ibrahim Ajibu.


Dk ya 23: Tshishimbi anapiga shuti linatola nje kidogo ya lango la Singida.
Dk ya 20: Biswita anacheza faulo. Inapigwa kueleka kwa Yang
Dk ya 16: Yanga wanafanya shambulizi kali, inakuwa kona.
Dk ya 15: Yanga wanafanya mashambulizi mawiali makali, wanapata kona mbili mfululizo.
Dk ya 14: Mchezo unaendelea.
Dk ya 12: Kipa wa Singida , Ally Mustapha 'Barthez' yupo chini ameumia wakati wa kurukia mpira.


Dk ya 10: Yusuph Mhilu anapiga shuti linamgonga beki na kuwa kona langoni mwa Singida.
Dk ya 9: Mpira umeganda kwenye lango la Yanga lakini walinzi wanakuwa makini kuzuia.
Dk ya 6: Singida wanapata mpira wa kurushwa pembeni ya uwanja.
Dk ya 4: Yanga ni kama bado hawajajipanga.
Krosi ya Kigi Makasi inatua mguuni kwa Saliti Kambale anamalizia wavuni.

Dk ya 2: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO


Dk ya 1: Yanga wanamiliki mpira, wanpiga pasi lakini Singida nao wapo makini.

Mchezo umeanza.
Mchezo unatarajiwa kuanza muda wowote kuanzia sasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic