April 17, 2018



Na George Mganga

Wakati homa ya watani wa jadi ikiendelea hivi sasa kwa mashabiki na wadau wa soka kwa ujumla kuelekea pambano la watani wa jadi, Simba na Yanga litakalopigwa Aprili 29 2018, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Nikufahamishe tu kuwa Yanga anaweza akaendelea kuutetea ubingwa wa ligi msimu huu.

Takwimu zinaonesha mpaka sasa Simba amecheza idadi ya mechi 24 huku akisaliwa na jumla ya michezo 6 ambayo ni sawa na pointi 18.

Wakati huo watani zake wa jadi, Yanga wao wameshacheza idadi ya michezo 22 huku wakiwa wamebakiza mechi 8 mkononi ambazo ni sawasawa na alama 24.

Kupitia takwimu hizo fupi inaonesha kuwa Yanga itaweza kuutwaa ubingwa wa ligi endapo itashinda michezo yake 8 iliyosalia.

Yanga atakuwa bingwa endapo Simba atapoteza michezo miwili kati ya 6 iliyobaki kwa kuwa atakuwa amefikisha pointi 70 badala ya 76.

Upande wa pili sasa, Yanga itautwaa ubingwa huo ikiwa itashinda mechi zote 8 zilizosalia baada ya Simba kupoteza michezo miwili kati ya 6, kwa maana itakuwa imefikisha alama 71 kwenye msimamo wa ligi.

Dawa ya pekee ya Simba kuchukua ubingwa wa ligi ambao imeukosa kwa misimu mitano mfululizo ni kushinda mechi 5 zilizosalia ambazo zitaifanya kuwa na alama 73 tofauti na Yanga itakayokuwa na 71 hata kama ikishinda mechi zake zote 8 zilizosalia.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic