April 5, 2018



Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Yanga umelitolea ufafanuzi suala la kuwaomba wanachama na wapenzi wa timu hiyo watakaoenda kuishangilia katika mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Welayta Dicha FC kuvaa jezi za njano badala ya kijani.

Zikiwa zimesalia siku kadhaa kuelekea mchezo huo, Yanga imekuwa ikihamasisha mashabiki wa timu hiyo kuvaa jezi hizo ambayo itafanya kung'arisha Uwanja huo dhidi ya wapinzani wao.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa timu hiyo, Dismas Ten, ameeleza kuwa rangi hiyo itaufanya uwanja huo kuwa na mng'aro mzuri ambao utatengeneza muonekano mzuri wa Uwanja, hivyo vema mashabiki wakavaa jezi za rangi hiyo.

Ten ameeleza hayo kupitia kipindi cha E Sports kinachorushwa na Radio EFM huku akiwaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia mechi hiyo.

Mchezo huo wa mkondo wa kwanza utapigwa Jumamosi ya Aprili 7 2018 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

2 COMMENTS:

  1. Nao wajitahidi kucheza mchezo utakaoendezesha watazamaji maana issue hapo ni give and take

    ReplyDelete
  2. Nguvu kubwa anayo tumia msemaji wa club ya yanga ya uvaaji jezi kwa mashabiki wa club ya yanga, Nguvu hiyo angeitumia kuwaambia ukweli watumie nafasi ya kushangilia kwa nguvu wasikae kimya na kusubir kushangilia baadhi ya matukio machache yanayo tokea uwanjani..

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic