Mwinyi Zahera ambaye Kocha Mkongomani wa Yanga ndiye aliyeuambia uongozi wa Yanga, anaweza kuanza kazi mara moja.
Zahera ameonekana anahitaji kuona anaongeza naye utaalamu wake wakati Yanga ikienda kuivaa Simba Jumapili.
Kocha huyo ameungana na wachezaji wa Yanga na kuanza kazi katika mazoezi ya Yanga mjini Morogoro.
"Kocha anaonekana si mtu mwenye kufanya mambo yawe magumu, amefika Morogoro na muda mchache akaungana na wachezaji na kuanza mazoezi," kilieleza chanzo.
Zahera aliwasili mjini Morogoro akitokea jijini Dar es Salaam, na muda mchache baadaye akaungana na wachezaji hao mazoezini.
Kocha huyo amejiunga na Yanga kuchukua nafasi ya George Lwandamina raia wa Zambia ambaye aliamua kurejea kwao kwa madai ya kutolipwa mishahara yake.
Yanga ipo mjini Morogoro kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba ambao sasa ndiyo vinara wa Ligi Kuu Bara.
0 COMMENTS:
Post a Comment