May 5, 2018



Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza kuwa familia ya Mshambuliaji wake, Ibrahim Ajibu, imejaaliwa kupata mtoto wa kike.

Ajibu alishindwa kusafiri na kikosi cha Yanga kuelekea Algiers, Algeria kwa ajili ya mechi ya mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya U.S.M Alger.

Mchezaji huyo amesema kuwa ujauzito wa mkewe umepitia changamoto mbalimbali, jambo lililopelekea hofu kubwa kwake lakini ameeleza kumshukuru Mungu kwa kufanikiwa kujifungua salama.

Mbali na mkewe kupata mtoto, Ajibu amesema kuwa ameumizwa na baadhi ya mashabiki waliomtumia ujumbe mfupi wa mane kupitia simu wakimuandama kuwa hajasafiri na timu.

"Nashukuru Mungu ametujaalia kupata mtoto wa kike, hapo kabla nilikuwa na hofu kubwa kwasababu ujauzito wa mke wangu ulikuwa na matatizo makubwa, kuna wakati nilikuwa nina hofu juu ya maisha yake.

"Naumizwa na wanaonishambulia kupitia sms kuwa nimegoma kuichezea timu, sina sababu ya kufanya hivyo maana mpira ni kazi yangu" amesema Ajibu.

Hata hivyo Ajibu hajasita kuwasamehe wote waliomshambulia kwa sms hizo kali pamoja na kumuandama katika mitandao mbalimbali ya kijamii, huku akieleza pengine kama wangesikia mke wake amefariki kwa matatizo ya uzazi, wangesema mengine.

"Nawasamehe kwasababu wangesikia mke wangu amefariki kwa matatizo ya uzazi, nadhani wangesema mengine" amesema Ajibu.














7 COMMENTS:

  1. Ukiwemo na Wewe Saleh uliokuwa unatuhabarisha kila kukicha kuwa amegoma Kusafiri.

    ReplyDelete
  2. Hongera sana ndugu yangu kwa kuongeza wanafamilia. Mungu amlinde na husda zote na ampe afya njema mama mtoto. Aamiyn

    ReplyDelete
  3. Mpira unahitaji mtu anayeweza kujitoa ajibu ni mchezaji wa show game hata mechi ikiwa ngumu na yenye umuhimu akijitoa sana ni asilimia 70 ila tu mi nichelee kumpa hongera ajaribu kutambua kuwa yeye anapaswa kutimiza malengo ya klabu ndio na yake yatimie

    ReplyDelete
  4. Hongera
    Mungu SW Amkuze vena mwanao kiakili kimwili na kiaqidah.
    Umlee vema katika dini

    ReplyDelete
  5. maa shaa Allah

    ReplyDelete
  6. Hongera Ajibu kwa kupata mtoto. Maneno kwa binadamu yatasemwa tu muhimu ni wewe mwenyewe na viongozi wako kwenye klabu na timu waelewe sababu zako za kutosafiri na timuyako.Umefanya vizuri sana kuthamini maisha ya mkeo na mtoto. Hongera sana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic