May 5, 2018



Na George Mganga


Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano katika klabu ya Simba, Haji Manara, amefunguka kwa kuwakosoa wale wanamdhihaki Mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu wakiwa na sababu zao binafsi.

Manara ameeleza kuwa kitendo cha baadhi ya mashabiki kumjadili na kumsema vibaya mchezaji huyo ni kukosa heshima iliyopitiliza.

Baadhi ya mashabiki wamekuwa wakimsema kwa mlengwa hasi Mshambuliaji huyo wakieleza kuwa ameshuka kiwango chake tofauti na namna kilivyokuwa mwanzoni mwa msimu pale ligi ilipoanza.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara ameandika kuwa kitendo hicho kinafaa kukemewa kwani kinaleta taswira tofauti kwa mchezaji kutokana na kauli ambazo hazina maana kwa Ajibu.

Mbali na hilo, Manara amemuelezea Ajibu kama mchezaji aliye na kipaji maridhawa na hai katika nchi hii pamoja na kumuelezea namna alivyoisaidia Yanga msimu huu.



Ajibu aliondoka Simba na kujiunga na Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa ligi ikiwa ni baada ya msimu wa 2016/17 kumalizika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic