May 22, 2018



Na George Mganga

Kikosi cha Yanga kimeondoa rekodi ya kushindwa kupata matokeo katika mechi 9 mfululizo zilizopita baada ya kuifunga Mbao FC kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi uliopigwa Uwanja wa Taifa jioni hii.

Bao pekee la mchezo huo limefungwa na kiungo Mzimbambwe, Thabn Kamusoko kwa njia ya faulo mnamo dakika ya 25 kipindi cha kwanza.

Matokeo hayo yameiongezea Yanga alama tatu muhimu kwa kufikisha pointi 51 zinazoipa Azam presha ya kuendelea kukalia nafasi ya pili ikitegemeana na matokeo ya mechi zilizosalia kwa timu zote mbili.

Ushindi huo wa Yanga umekuja mara baada ya kupoteza mechi nne mfululizo katika ligi ikiwa ni dhidi ya Simba, Prisons, Mwadui FC na Mtibwa Sugar.

ratiba inaonesha mchezo unaofuata kwa Yanga watakuwa wanaikaribisha Azam Fc katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, hivyo matokeo ya leo yamekuwa kama salaam kuelekea mechi hiyo kubwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic