May 30, 2018

Gassama (kulia) akipokea maelekezo kutoka kwa moja ya wafanyakazi wa kitengo cha zimamoto nchini Ufaransa
kuhusiana na utendaji kazi wa idara hiyo.


Kijana anayejulikana kwa jina la Mamadou Gassama, mzaliwa wa Mali, ameikataa ofa ya Rais wa nchi yake, Ibrahim Boubacar Keïta, aliyemtaka arejee kwao baada ya kupewa uraia wa Ufaransa.


Gassama alipewa uraia wa Ufaransa na Rais wa taifa hilo, Emmanuel Macron, baada ya kumuokoa mtoto aliyekuwa akining'inia gorofani kisha kupewa kazi katika idara ya zimamoto.

Baada ya Gassama kufanya tukio hilo la kishujaa kisha kumuokoa mtoto huyo, Rais Macron alimuita kijana huyo Ikulu na kufanya mazingumzo naye mafupi yaliyoambatana na kumpa uraia pamoja na kazi hiyo ya zimamoto.

Kitendo cha Gassama kupewa urais na kazi nchini Ufaransa kilimuibua Rais wa Mali na kumpa ofa aweze kurejea kwao huku akiahidi kumpa kazi katika kitengo cha Jeshi.

Gassama amekataa ofa hiyo na kusema tayari ameshakuwa Mfaransa na ataendelea kusihi huko kutokana na kuvutiwa na mazingira ya taifa hilo pamoja na kazi aliyopewa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic