May 16, 2018Na George Mganga

Leo Mei 16 2018 kikosi cha Yanga kinashuka dimbani kukipiga na Rayon Sports ya Rwanda katika mchezo wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga inacheza mchezo wa pili ikikumbuka kipigo kilichopita kwenye mashindano hayo dhidi ya USM Alger ya Algeria cha mabao 4-0.

Kuelekea mechi hiyo, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema wana majeruhu wengi lakini watapambana kupigania matokeo wapata alama tatu muhimu,

Akizungumza kupitia Spoti Leo ya Radio One, Zahera ameeleza kuwa hakuna jambo la msingi zaidi ya kusaka pointi tatu kutokana na kuharibu mechi ya kwanza huku wakiwa na majeruhi kadhaa.

Yanga inatakiwa kutumia Uwanja wake wa nyumbani vema ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kuelekea hatua ya nane bora.

Mechi hiyo itaanza majira ya saa 1 jioni kwenye Uwanja wa Taifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV